Ifahamu Wiliete Benguela Wapinzani wa Yanga CAF 2025/2026

Ifahamu Wiliete Benguela Wapinzani wa Yanga CAF 2025/2026

Miamba wa soka la Tanzania Bara na Visiwani Yanga SC, Simba SC, Azam FC, Singida Black Stars, KMKM, na Mlandege SC tayari wamepata majina ya wapinzani wao watakaokutana nao katika hatua ya awali ya kuzisaka tiketi za kufuzu makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) na Kombe la Shirikisho CAF msimu wa 2025/2026.

Droo ya upangaji wa mechi hizi ilifanyika Jumamosi iliyopita , ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika nchini Tanzania, tukio lililoshuhudiwa na magwiji wa soka wa miaka ya 1970 akiwemo Sunday Manara aliyewahi kung’ara na Yanga SC na Abdallah Kibadeni wa Simba SC.

Katika droo hiyo, mabingwa wa Ligi Kuu Bara Yanga SC wamepangwa kumenyana na Wiliete Benguela ya Angola, wakati Simba SC itaanza na Gaborone United ya Botswana, huku Mlandege SC wakianza dhidi ya Insurance ya Ethiopia.

Historia Fupi ya Wiliete Benguela

Wiliete Benguela ni klabu kutoka Jiji la Benguela, lililoko upande wa Magharibi mwa Angola. Hii ni timu changa kwenye ramani ya soka barani Afrika kwani ilianzishwa takribani miaka saba tu iliyopita, na msimu huu wa 2025/2026 ndio mara yao ya kwanza kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika. Walipata nafasi hii ya kihistoria baada ya kumaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya Angola msimu uliopita mafanikio yaliyowapa tiketi ya moja kwa moja kuiwakilisha nchi yao kwenye mashindano ya CAF.

Uwanja na Vifaa vya Michezo

Ingawa klabu hii inamiliki Uwanja wa Embaka wenye uwezo wa kuingiza mashabiki takribani 35,000, uwanja huo haujakidhi viwango vilivyowekwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa michezo ya Ligi ya Mabingwa. Kwa sababu hiyo, Wiliete Benguela imelazimika kutumia Uwanja wa Novemba 11 uliopo jijini Luanda kwa michezo yao ya nyumbani katika kampeni zijazo za CAF.

Wiliete Benguela hutumia jezi za rangi ya kijani wanapocheza nyumbani, rangi inayoendana na utambulisho wao wa klabu. Wakiwa ugenini, huvaa fulana nyeupe na bukta za kijani, muundo unaotoa mwonekano wa kipekee na wa kuvutia kwa wapenzi wa soka.

Benchi la Ufundi

Kwa sasa, timu hii inafundishwa na kocha Evaldo Tchissenda, ambaye ana jukumu kubwa la kuiongoza klabu hii changa kukabiliana na mabingwa wa Tanzania Yanga SC katika hatua ya awali. Changamoto hii itakuwa kipimo kikubwa kwa kikosi chake, hasa ikizingatiwa uzoefu mdogo wa klabu hii kwenye mashindano ya kimataifa.

Ifahamu Wiliete Benguela Wapinzani wa Yanga CAF 2025/2026

Mshindi wa michezo miwili kati ya Yanga SC na Wiliete Benguela atakutana na mshindi wa pambano kati ya Elgeco Plus ya Madagascar na Silver Strikers ya Malawi katika hatua inayofuata. Hii inamaanisha kila timu italazimika kuonesha ubora mapema ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Msimamo wa Makundi CHAN 2025
  2. Ratiba ya Mechi za Leo 12/08/2025 CHAN
  3. Ratiba ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2025/2026
  4. Yanga Kucheza Mechi ya Kirafiki Dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda 15/08/2025
  5. Everton na Man City Wakubaliana Kuhusu Uhamisho wa Mkopo wa Grealish
  6. Wachezaji Wapya wa Yanga 2025/2026
  7. Vilabu Bora Afrika 2025 (CAF Club Ranking 2025)
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo