Yanga Yampa Farid Mussa Mkataba wa Miaka Miwili Zaidi
Mabingwa wa Ligi kuu ya NBC Tanzania na CRDB bank confederation cuo Yanga SC, wametangaza Farid Mussa Malick kuendelea kubakia ndani ya viunga vya Jangwani kwa kipindi kingine cha miaka miwili, mkataba utakaomuweka ndani ya timu hadi mwaka 2026. Nyota huyu wa Kitanzania, ambaye amejiunga na klabu ya Yanga SC mwaka 2020, amekuwa nguzo muhimu katika mafanikio ya timu.
Fundi wa Boli Faridi Mussa Shaha bado yupo sana Jangwani📄✍️✅
Taarifa kamili inapatikana Yanga SC APP📲#TimuYaWananchi #DaimaMbeleNyumaMwiko pic.twitter.com/vxuQ5nVqSw
— Young Africans SC (@YoungAfricansSC) July 1, 2024
Historia ya Farid Mussa na Yanga SC
Farid Mussa alijiunga na klabu ya Yanga SC baada ya janga la Corona kuvuruga mipango yake ya kurejea Hispania kwa ajili ya kucheza soka la kulipwa. Kabla ya kujiunga na Yanga, kulikuwa na tetesi kwamba Simba SC walikuwa wakimhitaji zaidi, lakini nafasi yake ilionekana kuwa finyu kutokana na uwepo wa Clatous Chama, kiungo ambaye alikuwa katika kiwango cha juu wakati huo. Hii ilimlazimu Farid kutafuta nafasi nyingine, na hivyo kujiunga na mabingwa wa mitaa ya jangwani Yanga SC.
Tangu kujiunga na Yanga, Farid Mussa amekuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya timu. Ameisaidia klabu kutwaa mataji ya Ligi Kuu Tanzania Bara mara tatu, Ngao ya Jamii mara mbili, na Kombe la Shirikisho FA mara tatu.
Pia, Farid alikuwa sehemu muhimu ya timu iliyofika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na kufikia hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika msimu uliopita.
Farid Mussa, ambaye anavaa jezi namba 17 katika Yanga, anajulikana kwa uwezo wake wa kucheza kama winga na pia kama kiungo.
Uwezo huu wa kucheza nafasi tofauti unampa thamani kubwa katika kikosi cha Yanga, na ni moja ya sababu zilizomfanya klabu hiyo kumuongezea mkataba.
Katika kipindi chake na Yanga, Farid ameonyesha kuwa mchezaji wa kutegemewa, akionyesha ustadi na juhudi katika kila mechi.
Kama ilivyokuwa kwa Farid Mussa, Yanga SC imeendelea kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali, na kuongeza mkataba wake ni ishara ya kuendelea kwa dhamira ya klabu hiyo kufikia mafanikio zaidi.
Katika msimu uliopita, Yanga ilifikia hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika CAF, na mashabiki wengi sasa wanatarajia kuona timu ikifanya vizuri zaidi katika mashindano yajayo.
Maoni ya Farid Mussa Kuhusu Mkataba Mpya
Akizungumzia kuhusu kuongeza mkataba wake na klabu ya Yanga Sc, Farid Mussa alionyesha furaha yake na kusema kuwa anatarajia kuendelea kutoa mchango mkubwa zaidi kwa timu yake. “Nina furaha kuendelea kuwa sehemu ya familia ya Yanga SC. Ninaamini tunaweza kufikia mafanikio makubwa zaidi katika miaka ijayo,” alisema Farid.
Mapendekezo Ya Mhariri:
- Azam Fc Yakubali Ombi La Prince Dube Kuvunja Mkataba
- Wachezaji Walio Ongeza Mkataba Simba 2024/2025
- Yanga Yafukuzisha Kocha Mamelodi Sundowns
- Jean Charles Ahoua Kurithi Mikoba ya Chama Simba 2024/2025
- Mishahara ya Wachezaji wa Yanga sc 2024
- Cv Ya Joshua Mutale Mchezaji wa Simba
- Singida Black Stars Yawinda Sahihi ya Zawadi Mauya
- Wachezaji Wapya Azam 2024/2025 (Wachezaji Waliosajiliwa Azam FC)
- Azam Yatuma Ofa Kwa Simba Kumsajili Kipa Aishi Manula
- Tetesi za Usajili simba 2024/2025
Weka Komenti