Kikosi cha Tanzania vs Guinea leo 19/11/2024 | Kikosi cha Taifa Stars leo Vs Guinea
Leo, Stars itashuka dimbani kucheza mchezo wa mwisho wa kufuzu michuano ya mataifa Afrika Afcon 2025 dhidi ya Guinea kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa utakaoanza saa 10:00 jioni. Mchezo huu ndio utaamua nani anaendelea na safari kati ya Tanzania na Guinea, ambao wote wanapambana kupata tiketi iliyosalia ya kundi H, baada ya DR Congo tayari kubeba tiketi ya kwanza.
Kwa Taifa Stars, ushindi pekee ndio njia ya kufanikisha ndoto ya kufuzu kwa mara ya nne katika historia, huku matumaini makubwa yakiwekwa kwa mastaa wakuu kama Mbwana Samatta, Simon Msuva, na Feisal Salum.
Katika Kundi H, DR Congo tayari imefuzu ikiwa na alama 12, huku Ethiopia ikishika mkia na alama moja. Stars ina pointi 7, wakati Guinea ina pointi 9. Kwa hesabu hizi, Tanzania inahitaji ushindi wa moja kwa moja ili kuipiku Guinea na kutwaa nafasi ya pili.
Kaimu Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Hemed Suleiman ‘Morocco’, ameweka wazi kuwa maandalizi ya timu yako vizuri, huku akisisitiza kwamba wachezaji wote wapo fiti na tayari kwa changamoto hii kubwa.
Nahodha wa timu, Mbwana Samatta, pamoja na mshambuliaji, Simon Msuva, wanatarajiwa kuwa nguzo muhimu. Wawili hawa walikuwa sehemu ya ushindi muhimu dhidi ya Ethiopia, ambapo Samatta na Msuva walionyesha ubora wao uwanjani.
Msuva, akiwa na mabao 23 katika michezo 93, ana nafasi ya kuvunja rekodi ya Mrisho Ngassa, aliyefunga mabao 25 katika mechi 100. Naye Samatta ana mabao 22 katika michezo 82 na ni miongoni mwa washambuliaji bora katika historia ya timu ya taifa.
Kwa upande wa Guinea, kikosi chao kinategemea sana mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Serhou Guirassy, aliyefunga mabao sita katika mechi tatu zilizopita. Safu ya ulinzi ya Taifa Stars, ikiongozwa na Ibrahim Bacca na Dickson Job, ina jukumu zito la kuhakikisha Guirassy hana nafasi ya kuonyesha uwezo wake.Kwa mujibu wa kipa Aishi Manula, Taifa Stars imefanya uchambuzi wa kina wa timu ya Guinea na mbinu za kuwakabili wapinzani hao zipo tayari.
Kikosi cha Tanzania vs Guinea leo 19/11/2024
Kikosi rasmi cha Timu ya Taifa ya Tanzania kitakachoshiriki kwenye mchezo dhidi ya Guinea kinatarajiwa kutangazwa na Kocha Morrocco saa moja kabla ya mtanange kuanza. Hapa tutakuletea orodha kamili ya wachezaji watakaoanza kuiwakilisha na kuipigania Tanzania mara tu kikosi kitakapotangazwa na kocha.
Historia na Matarajio ya Taifa Stars
Tanzania imewahi kufuzu mara tatu katika michuano ya AFCON (1980, 2019, na 2024). Mchezo wa leo si tu wa kuwania tiketi ya 2025, bali pia ni nafasi ya kulinda heshima mbele ya mashabiki wake nyumbani. Katika mchezo wa kwanza, Stars ilishinda 2-1 dhidi ya Guinea ugenini, matokeo ambayo yanatoa matumaini makubwa kwa mchezo wa leo. Kwa Guinea, sare pekee inawatosha kufuzu, lakini Taifa Stars ina rekodi ya kuzidiwa nyumbani katika mechi za hivi karibuni, jambo linalohitaji kubadilishwa leo.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Fadlu Davids Afurahishwa Kurejeshwa Kwa Mechi Dhidi ya Pamba Kabla ya CAFCC
- Aussems Ampa Madini Guede
- Viingilio Mechi Ya Yanga VS Yanga Vs Al Hilal 26/11/2024
- Vituo Vya Kununua Tiketi Mechi ya Yanga Vs Al Hilal 26/11/2024
- Moto wa Tabora United Wawashinikiza Singida BS Kutafuta Mechi ya Kirafiki
- Mastaa Ligi Kuu Bara Waongoza Nchi Zao Kufuzu Afcon
Leave a Reply