Lawi Ndani ya Kikosi cha Coastal Union Dhidi ya Mashujaa
HATIMAYE beki Lameck Lawi ameibuka kwenye kikosi ya Coastal Union kinachotarajia kushuka dimbani kukabiliani na Mashujaa katika mechi ya Ligi Kuu Bara inayopigwa kwenye Uwanja wa KMC Complex. Hii ni habari njema kwa mashabiki wa Coastal Union ambao wamekuwa wakimsubiri kwa hamu beki huyu mahiri arejee uwanjani.
Coastal Union, wenyeji wa mchezo huu, watakuwa wakicheza mchezo wao wa pili msimu huu, huku Mashujaa wakiwa wameshacheza michezo mitatu. Katika mchezo wao wa kwanza, Coastal Union walilazimishwa sare ya 1-1 na KMC, wakati Mashujaa walianza kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji kabla ya kutoka sare tasa na Pamba.
Lawi, ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu akisubiri uamuzi wa Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya TFF kutokana na kuhusishwa na kusaini mkataba na Simba, sasa amerudi kikosini. Beki huyu alikuwa msaada mkubwa kwa Coastal Union msimu uliopita, akiwasaidia kumaliza katika nafasi ya nne na kufuzu kwa Kombe la Shirikisho Afrika.
Baada ya kutimkia Gent A.A.K kwa ajili ya mazungumzo ya kujiunga na timu hiyo, Lawi alirejea nchini na hakuweza kucheza mechi mbili za kwanza za Coastal Union msimu huu huku akisubiri uamuzi kuhusu mustakabali wake.
Kikosi cha Coastal Union Dhidi ya Mashujaa
Leo, jina la Lawi limeibuka katika orodha ya wachezaji 11 wa kikosi kinachotarajiwa kuanza dhidi ya Mashujaa. Wengine katika kikosi hicho ni pamoja na kipa Ley Matampi, Jackson Shiga, Miraji Adamu, Mukrim Issa, Anguti Luis, Abdallah Hassan, Lucas Kikoti, John Makwattar, Mbaraka Yusuph na Hernest Briyock Malonga.
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti