Majina ya Waliopata Mkopo HESLB Awamu ya Pili 2024/2025 | Majina ya Wanufaika wa Mkopo HESLB Awamu ya Pili
Majina ya Waliopata Mkopo HESLB Awamu ya Pili 2024/2025
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza awamu ya pili ya orodha ya wanafunzi waliofanikiwa kupata mkopo kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2024/2025. Tangazo hili muhimu limetolewa leo Jumatano, tarehe 9 Oktoba, 2024, na linawahusu wanafunzi wa ngazi mbalimbali za elimu ya juu, kuanzia shahada ya kwanza, stashahada (diploma), shahada ya uzamili, hadi shahada ya uzamivu. Awamu hii ya pili inafuatia awamu ya kwanza iliyotangazwa mwezi Septemba, na inalenga kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wenye sifa wanapata fursa ya kupata mkopo ili kutimiza ndoto zao za kielimu.
Wanafunzi 30,311 wapata mikopo ya shahada ya kwanza
Katika awamu hii ya pili, wanafunzi 30,311 wa shahada ya kwanza wamepangiwa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 93.7. Idadi hii inafanya jumla ya wanafunzi waliopata mikopo kwa awamu ya kwanza na ya pili kufikia 51,645, na jumla ya thamani ya mikopo hiyo ni shilingi bilioni 163.8. Kati ya wanafunzi hawa, 43% ni wa kike na 57% ni wa kiume.
Wanafunzi 2,157 wapata mikopo ya stashahada (diploma)
Aidha, wanafunzi 2,157 wa stashahada (diploma) wamepangiwa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 5.6.
Wanafunzi wa shahada ya uzamili na uzamivu nao wanufaika
Wanafunzi 45 wa shahada ya uzamili wamepata mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 205.6, na wanafunzi 16 wa shahada ya uzamivu wamepata mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 215.6.
Awamu ya Tatu ya Mikopo Inatarajiwa Kutangazwa Hivi Karibuni
HESLB inaendelea kupokea taarifa za udahili kutoka vyuo mbalimbali ili kuwezesha upangaji wa mikopo kwa awamu ya tatu. Awamu hii inatarajiwa kutangazwa siku chache zijazo.
Samia Scholarship yawanufaisha wanafunzi 588: Wanafunzi 588 wa shahada ya kwanza wamepata ufadhili wa ‘Samia Scholarship’ kwa mwaka wa masomo 2024/2025. Ufadhili huu, wenye thamani ya shilingi bilioni 2.9, unalenga wanafunzi wenye ufaulu wa juu katika masomo ya sayansi, teknolojia, uhandisi, hisabati, na sayansi za tiba.
Jinsi ya Kuangalia Mkopo HESLB Awamu ya Pili 2024/2025
Wanafunzi ambao wameomba mkopo wa elimu ya juu kupitia HESLB wanaweza kufuatilia majibu ya maombi ya mkopo HESLB kwa njia ya kupitia akaunti yao ya SIPA HESLB . Njia hii ni rahisi na zinatoa taarifa sahihi kuhusu kama mwanafunzi amepata mkopo au la.
Kuangalia Kupitia Akaunti ya SIPA (Student’s Individual Permanent Account)
HESLB inatumia mfumo wa SIPA kwa ajili ya wanafunzi wote waliotuma maombi ya mkopo. Akaunti ya SIPA ni akaunti binafsi ambayo kila mwanafunzi hujipatia wakati wa kuomba mkopo. Ili kuangalia kama umepata mkopo, fuata hatua hizi:
Fungua Tovuti ya HESLB: Tembelea tovuti rasmi ya HESLB au bonyeza moja kwa moja kwenye kiungo hiki https://olas.heslb.go.tz/olams/account/login.
Ingia kwenye Akaunti yako: Tumia jina la mtumiaji na nenosiri ulilojisajili nalo wakati wa kuomba mkopo.
Mara Baada ya kuingia katika akaunti yako, Bofya Kitufe kilichoandikwa “SIPA” Kisho Bofya “ALLOCATION”
Chagua mwaka wa masomo. Baada ya kubofya “Allocation” Utapelekwa kwenye ukurasa mwengine ambapo unatakiwa kuchagua mwaka wa masomo (2024/2025) ili kuweza kuona kiasi cha mkopo ulicho pata.
Angalia Taarifa zako za Mkopo: Utaweza kuona kama umepewa mkopo na kiasi kilichopangiwa. Ni muhimu kufuatilia akaunti yako mara kwa mara ili kujua hali ya maombi yako. Mabadiliko yoyote yanayohusiana na mkopo yataonekana ndani ya akaunti yako ya SIPA.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Ratiba ya Mtihani wa Kidato cha Pili 2024
- Matokeo Ya Uhakiki Nactevet Waombaji Waliochaguliwa Awamu Ya Pili Septemba 2024/2025
- Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga Vyuo vikuu Awamu ya Pili 2024/2025
- Majina ya Waliochaguliwa Chuo Cha UDSM Awamu ya Pili 2024/2025
- Majina ya Waliochaguliwa Chuo Kikuu Cha UDOM Awamu ya Pili 2024/2025
- Dirisha la Tatu la Maombi ya Vyuo Vikuu 2024/25: Tarehe 05 – 09 Oktoba
- Majina ya Waliochaguliwa kujiunga Chuo Kikuu Cha UDSM 2024/2025
Leave a Reply