Idadi ya Makombe ya UEFA Real Madrid | Jumla ya Makombe ya Klabu Bingwa Ulaya ya Real Madrid
Real Madrid, wababe wa soka kutoka Hispania, imeendeleza utawala wake katika soka la Ulaya kwa kutwaa kombe la 15 la Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League) baada ya kuifunga Borussia Dortmund kwenye fainali ya kusisimua iliyofanyika Uwanja wa Wembley June 01 2024.
Ushindi huu ni wa sita kwa Real Madrid ndani ya miaka kumi iliyopita, na unathibitisha zaidi nafasi yao kama timu yenye mafanikio makubwa katika historia ya mashindano haya ya kifahari. Timu hiyo ya Hispania ilionyesha ubabe wao uwanjani kwa mchezo wa kusisimua na ushindi wa kishindo. Los Blancos, kama wanavyojulikana, walikuwa na mfululizo wa ushindi katika mashindano haya, wakishinda kila mchezo tangu hatua ya makundi. Ubora wao uwanjani na uzoefu katika mechi kubwa uliwapa faida kubwa dhidi ya Borussia Dortmund.
Idadi ya Makombe ya UEFA Real Madrid
Real Madrid imekuwa na utawala mkubwa katika soka ya Ulaya, hasa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya. Wameshiriki katika fainali 18, wakishinda 15 na kupoteza tatu pekee. Idadi hii ya mataji ni mara mbili ya AC Milan, timu iliyopo nafasi ya pili kwa mataji mengi.
Hii apa Orodha ya Misimu ambayo Real Madrid ameshinda UEFA
Sn | SEASON | WINNER |
15 | 2023-24 | Real Madrid |
14 | 2021-22 | Real Madrid |
13 | 2017-18 | Real Madrid |
12 | 2016-17 | Real Madrid |
11 | 2015-16 | Real Madrid |
10 | 2013-14 | Real Madrid |
9 | 2001-02 | Real Madrid |
8 | 1999-2000 | Real Madrid |
7 | 1997-98 | Real Madrid |
6 | 1965-66 | Real Madrid |
5 | 1959-60 | Real Madrid |
4 | 1958-59 | Real Madrid |
3 | 1957-58 | Real Madrid |
2 | 1956-57 | Real Madrid |
1 | 1955-56 | Real Madrid |
Mapendekezo Ya Mhariri:
- Viingilio vya Fainali ya Kombe la Shirikisho CRDB 2024: Bei na Maeneo ya Kununua Tiketi Yatangazwa!
- Ley Matampi Golikipa mwenye Clean Sheet Nyingi Ligi Kuu NBC 2023/2024
- Timu za Tanzania Zilizofuzu Klabu Bingwa Afrika 2024/2025
- Timu Zilizofuzu Klabu Bingwa Afrika 2024/2025
- Muonekano wa Kombe La CRDB Federation Cup 2023/2024
- Harry Kane Ndio Mshindi wa Kiatu cha Dhahabu Ulaya 2023-2024
Weka Komenti