Makundi ya CECAFA Kagame Cup 2025

Makundi ya CECAFA Kagame Cup 2025

Michuano ya CECAFA Kagame Cup 2025 inatarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia Septemba 2 hadi 15 jijini Dar es Salaam, ikiwa ni mara nyingine tena Tanzania inakuwa mwenyeji wa mashindano haya makubwa ya klabu za Afrika Mashariki na Kati.

Mashindano haya yamepangwa kufanyika katika viwanja vitatu vya mkoa wa Dar es Salaam ambavyo ni Azam Complex (Chamazi), KMC Complex (Mwenge) na Uwanja wa Meja Jenerali Isamuyo (Mbweni).

Droo ya upangaji wa makundi imefanyika Agosti 28, 2025 katika hoteli ya Pan Pacific Suites jijini Nairobi, na kuzikutanisha klabu 11 kutoka nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

Makundi ya CECAFA Kagame Cup 2025

Kwa mujibu wa droo hiyo, timu shiriki zimegawanywa katika makundi matatu kama ifuatavyo:

Kundi A

  1. Singida Black Stars FC (Tanzania)
  2. Garde Cotes FC (Djibouti)
  3. Ethiopian Coffee SC (Ethiopia)
  4. Kenya Police FC (Kenya)

Kundi B

  1. APR FC (Rwanda)
  2. NEC FC (Uganda)
  3. Bumamuru FC (Burundi)
  4. Mlandege FC (Zanzibar)

Kundi C

  1. Al Hilal SC (Sudan)
  2. Kator FC (Sudan Kusini)
  3. Mogadishu City Club (Somalia)
  4. Al Ahly SC Wad Madani (Sudan)

Makundi ya CECAFA Kagame Cup 2025

Udhamini na Thamani ya Mashindano

Mashindano ya mwaka huu yamepata udhamini mpya kutoka kampuni ya michezo ya kubashiri Betika, ambayo imetangaza kuwekeza Shilingi milioni 42 za Kenya (sawa na zaidi ya Shilingi milioni 814 za Kitanzania). Kiasi hiki kinaifanya Kagame Cup 2025 kuwa na thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 800, hatua inayoongeza hamasa na hadhi ya mashindano haya ya muda mrefu.

Makamu wa Rais wa CECAFA, Paulos Weldehaimanot, alisema udhamini huu ni kielelezo cha mshikamano kati ya sekta binafsi na michezo, huku akisisitiza kuwa mchango wa Betika unaonyesha imani kubwa katika maendeleo ya soka la ukanda huu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Betika, Mutua Mutawa, alisema kampuni yake inajivunia kushiriki kwenye safari ya kukuza vipaji vya soka la Afrika Mashariki na Kati kupitia mashindano haya.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Simba Yamtambulisha Selemani Mwalimu Kutoka Wydad AC kwa Mkopo wa Mwaka
  2. Simba Kuivaa Gor Mahia ya Kenya Kwenye Kilele cha Simba Day
  3. Mshambuliaji Clement Mzize Asaini Kuendelea na Yanga Hadi 2027
  4. Opah Clement Atambulishwa Rasmi SD Eibar ya Hispania
  5. Yanga SC Kucheza Dhidi ya Bandari FC Siku ya Wiki ya Mwananchi
  6. Morocco Yatinga Fainali ya CHAN Baada ya Kuifunga Senegal kwa Penalti
  7. Madagascar Kukipiga Dhidi ya Morocco Fainali ya CHAN 2025
  8. Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2025/2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo