Manchester City washindwa kutamba dhidi ya Inter

Manchester City washindwa kutamba dhidi ya Inter

Klabu ya Manchester City, mabingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza, walishindwa kutamba dhidi ya mabingwa wa Italia, Inter Milan, katika mechi yao ya ufunguzi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Mechi hiyo iliyopigwa usiku wa Jumatano iliishia kwa sare tasa (0-0), huku Manchester City wakikosa kutumia nafasi walizozipata dhidi ya ulinzi madhubuti wa Inter Milan.

Mechi hii imeibua hisia mseto, hasa baada ya Manchester City kuwafunga Inter Milan kwa ushindi mwembamba katika fainali ya Ligi ya Mabingwa mwaka 2023. Wengi walitarajia City wangetamba katika mechi hii ya ufunguzi, lakini ulinzi wa Inter ulionesha uimara mkubwa na kuwazima washambuliaji hatari wa City.

Manchester City wakosa makali mbele ya Ulinzi wa Inter Milan

Timu zote zilionesha uwezo mkubwa uwanjani, lakini zilishindwa kutumia vyema nafasi walizotengeneza.

Timu ya Pep Guardiola, licha ya kutawala sehemu kubwa ya mchezo, ilikumbana na changamoto ya kuifungua safu ya ulinzi ya Inter, iliyokuwa imepangwa kwa nidhamu kubwa na kocha Simone Inzaghi.

Mashambulizi ya City yaliendeshwa na mastaa kama Erling Haaland na Jack Grealish, lakini kila juhudi yao ilizimwa na mabeki wa Inter, huku kipa wao, Yann Sommer, akifanya kazi nzuri kuhakikisha lango lake halifungwi. Haaland alijaribu mara kadhaa kufunga, lakini ulinzi wa Inter ulifanya kila liwezekanalo kumzuia nyota huyo kuleta madhara.

Manchester City washindwa kutamba dhidi ya Inter

Inter Milan yakosa makali katika kumalizia mashambulizi

Kwa upande mwingine, Inter Milan walionekana kupambana vikali lakini walikosa umakini wa kumalizia mashambulizi yao. Ingawa walifanikiwa kuupenya ulinzi wa Manchester City mara kadhaa, safu yao ya ushambuliaji ikiongozwa na Lautaro Martinez ilishindwa kutikisa nyavu za kipa Ederson.

Mashabiki wa Inter walitarajia ushindi kutokana na nafasi walizozipata, lakini tatizo la umaliziaji likawa kikwazo kikubwa. Licha ya safu ya kiungo na mabeki wa City kufanya kazi ya ziada kuzuia mashambulizi, Inter walikuwa na nafasi kadhaa nzuri za kufunga, lakini uzembe katika kumalizia ulikwamisha ndoto ya kupata ushindi.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Arsenal Yaambulia Pointi Moja Ugenini, Raya Aokoa Mkwaju wa Penalti
  2. Msimamo NBC Premier league 2024/2025 | Ligi Kuu Bara
  3. Gadiel Aanza Kazi Chippa United, Majogoro Kicheko
  4. Azam FC Yaichapa KMC 4-0, Taoussi Aanza Kugawa Dozi
  5. Wataalam wa Soka Wachambua Utofauti wa Dube na Baleke
  6. Tanzania Ipo Nafasi ya Ngapi Viwango vya FIFA 2024
  7. Viwango vya FIFA Afrika 2024 Timu za Taifa
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo