Msimamo NBC Premier league 2024/2025 | Msimamo Ligi Kuu Bara | Msimamo Wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2024-2025
Msimu wa 2023/2024 wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania umekamilika kwa kishindo, Yanga SC wakiibuka mabingwa kwa mara ya tatu mfululizo. Wanajangwani hao walimaliza kileleni mwa msimamo wakiwa na pointi 80 baada ya kucheza mechi 30, wakishinda mechi 26, wakitoa sare mbili, na kupoteza mbili pekee. Azam FC na Simba SC walimaliza nafasi ya pili na ya tatu mtawalia, zote zikiwa na pointi 69, huku Azam FC ikiwazidi Simba kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Msimu wa 2024/2025 unatarajiwa kuwa na mvuto mkubwa zaidi, huku timu zikifanya usajili wa nguvu na kujiandaa kwa ajili ya kuwania taji la ubingwa. Je, Yanga SC wataweza kutetea ubingwa wao?
Azam FC na Simba SC zitaweza kuwashusha Yanga kutoka kileleni? Je, tutashuhudia timu zingine zikiibuka na kuwa miongoni mwa washindani wakuu? Maswali haya na mengine mengi yatajibiwa kadri msimu huu utakavyokuwa ukiendelea.
Mashabiki wa soka Tanzania wana kila sababu ya kutazamia msimu uliojaa msisimko, ushindani mkali, na mshangao mwingi. Ligi Kuu ya NBC 2024/2025 inaahidi kuwa msimu ambao hautakumbukwa tu kwa matokeo yake, bali pia kwa ubora wa soka litakalochezwa.
Msimamo NBC Premier league 2024/2025 | Ligi Kuu Bara
- MP- Michezo Iliyochezwa (Match Played)
- W- Ushindi (Winsi)
- D- Sare (Draw)
- L-Kufungwa (Lose)
- GF- Magoli Ambayo Timu Imefunga (Goal For)
- GA- Magoli Ambayo Timu Imefungwa (Goals Against)
- GD- Tofauti Ya Magoli (Goal Difference)
- PTS- Jumla Ya Alama (Points)
Mapendekezo Ya Mhariri:
Weka Komenti