Matokeo ya Simba Vs Singida Black Stars Leo 31/05/2025 | Matokeo ya Simba Leo Dhidi ya Singida BS Nusu Fainali
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, leo tarehe 31 Mei 2025, wanatarajiwa kushuka dimbani kuisaka tiketi ya kutinga fainali nyingine ya Kombe la Shirikisho la CRDB ā baada ya safari yao kukwama kwenye hatua ya juu ya michuano ya CAF.
Mchezo huu wa nusu fainali utapigwa majira ya saa 9:30 alasiri katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, ukikutanisha vigogo wa soka ā Simba SC dhidi ya Singida Black Stars, timu inayokuja kwa kasi msimu huu. Simba SC wanaingia katika mchezo huu wakitambua kuwa ushindi utafungua ukurasa mpya wa Kariakoo Derby kwenye fainali, kwani Yanga SC tayari wamefuzu baada ya kuingāoa JKT Tanzania. Hii ni nafasi kwa Simba kurejesha heshima yao ndani ya nchi baada ya kutofikia malengo katika michuano ya CAF. Kwa upande wa Singida Black Stars, hii ni nafasi adimu ya kutikisa historia, kwani hawajawahi kuwafunga Simba SC kwenye mechi yoyote ya mashindano.
Matokeo ya Simba Vs Singida Black Stars Leo 31/05/2025
Simba Sc | VS | Singida BS |
Rekodi Ya Simba SC Dhidi ya Singida Black Stars
Timu hizi zimekutana mara 9 kwenye mashindano yote, huku Simba ikishinda mara 8 na kutoa sare mara moja ā bila kupoteza hata mchezo mmoja. Hili linaipa Simba hali ya kujiamini lakini pia linaongeza presha kwa Singida kuonesha ubadiliko wa matokeo.
Kwa msimu huu wa 2024/25, mechi zao mbili zilizopita zilimalizika kwa ushindi wa Simba:
- Singida Black Stars 0-1 Simba SC ā bao la kichwa kutoka kwa Fabrince Ngoma.
- Simba SC 1-0 Singida Black Stars ā bao safi la Steven Mukwala.
Nyota Wa Kuangaliwa Leo
Jean Ahoua, kiungo mshambuliaji wa Simba SC, ndiye amekuwa mwiba mkubwa kwa Singida Black Stars msimu huu. Ametengeneza mabao yote yaliyofungwa dhidi yao kwa msimu huu na ana pasi 8 za mabao katika ligi. Leo, macho yote yako kwake.
Kwa upande wa Singida Black Stars, Jonathan Sowah ndiye mchezaji anayeibeba safu yao ya ushambuliaji akiwa na mabao 11 hadi sasa. Anaweza kuwa tishio kwa ngome ya Simba kama akipata nafasi.
Kelvin Nashon, kiungo mkabaji wa Singida, pia anatarajiwa kuwa na kazi ngumu dhidi ya kina Ahoua na Kapombe. Rekodi yake ya kupata kadi za njano inapojaribu kuwadhibiti wachezaji wa Simba inaonesha jinsi mchezo huu utakavyokuwa mkali.
Matokeo ya Mhariri:
- Kikosi cha Simba Vs Singida Black Stars Leo 31/05/2025
- Simba Vs Singida Black Stars Leo 31/05/2025 Saa Ngapi?
- Coastal Union Yapiga Hesabu Kali Kumchukua Anicet Kiazayidi
- Chelsea Yaipiga Bao Manchester United Usajili wa Liam Rory Delap
- Xabi Alonso Aahidi Kurejesha Ufalme wa Real Madrid
- Singida BS Yashindwa Kutamba Mbele ya Simba Ligi Kuu NBC
- Waliochaguliwa JKT Mujibu wa Sheria 2025 ā Pakua PDF Hapa!
- Erik Ten Hag Atambulisha Rasmi Kama Kocha Mkuu Bayer Leverkusen
Leave a Reply