Matokeo ya Yanga vs Wiliete SC Leo 27/09/2025

Matokeo ya Yanga vs Wiliete SC Leo 27/09/2025

Safari ya kusaka tiketi ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika CAF inaendelea kwa kishindo. Wikiendi hii macho ya mashabiki wa soka Tanzania yameelekezwa jijini Dar es Salaam, ambapo Young Africans SC (Yanga) watashuka dimbani kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kuwakabili Wiliete SC ya Angola katika mchezo wa marudiano.

Mabao matatu waliyoibuka nayo ugenini wiki iliyopita yamewapa nafasi kubwa ya kufuzu hatua inayofuata, lakini mchezo wa leo, Jumamosi 27 Septemba 2025, utakuwa kipimo cha kuthibitisha ubora wao mbele ya mashabiki wao wa nyumbani.

Mashabiki wa Yanga Sc wanatarajia kuona timu yao ikikamilisha kazi iliyoanzishwa Benguela. Kocha Romain Folz ameweka wazi kuwa kikosi chake hakitategemea matokeo ya awali pekee, bali kitaingia na lengo la kushinda tena nyumbani.

Kwa upande mwingine, Wiliete SC chini ya kocha Bruno Ferry wamesema hawatakuja “kupaki basi.” Badala yake, watajaribu kushambulia mwanzo hadi mwisho ili kupata mabao ya mapema yanayoweza kubadili matokeo ya jumla.

Matokeo ya Yanga vs Wiliete SC Leo 27/09/2025

Yanga Sc 2-0 Wiliete SC

Taarifa Kuhusu Mechi

🏆 #CAFCL
🆚 Wiliete SC
🗓️ 27 Sept 2025
🏟️ Benjamin Mkapa
⏱️ Saa 11:00 Jioni

Matokeo ya Yanga vs Wiliete SC Leo 27/09/2025

Umuhimu wa Mechi ya Leo

Mshindi wa jumla kati ya Yanga vs Wiliete SC ataendelea kwenye raundi inayofuata kuwania tiketi ya hatua ya makundi. Huko atakutana na mshindi kati ya Elgeco Plus ya Madagascar na Silver Striker ya Malawi.

Kwa Yanga, hii ni nafasi muhimu ya kuendeleza safari yao kwenye michuano mikubwa barani Afrika, kuongeza heshima ya klabu na kuonyesha ubora wa soka la Tanzania.

Form ya Yanga Kabla ya Mchezo

Kabla ya marudiano ya leo, Yanga imecheza michezo mitatu ya mashindano msimu huu na haijaruhusu bao lolote:

  • Ushindi 1-0 dhidi ya Simba SC (Ngao ya Jamii).
  • Ushindi 3-0 dhidi ya Wiliete SC (mchezo wa kwanza).
  • Ushindi 3-0 dhidi ya Pamba Jiji (Ligi Kuu NBC).

Hali hii inawapa mashabiki matumaini kwamba kikosi kipo imara kutafuta ushindi mwingine nyumbani.

Mapendekezo ya Mhariri:

Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo