Yanga SC Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania 2023/24: Ushindi wa Mara ya 30 Kihistoria
- Dar es Salaam, Tanzania – Klabu ya soka ya Yanga SC imeandika historia kwa mara nyingine tena baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) msimu wa 2023/24. Ushindi huu wa kihistoria unaashiria mara ya 30 Yanga SC kutwaa taji hili, na kuimarisha utawala wao katika soka la Tanzania.
Yanga SC Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania 2023/24
Yanga SC walitawazwa mabingwa rasmi may 13 2024 baada ya ushindi wa kusisimua wa 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Manungu Complex, Turiani, Morogoro. Licha ya Mtibwa Sugar kutangulia kwa bao la Charles Ilamfya dakika ya 32, Yanga walipambana na kusawazisha kupitia kwa Mzambia Kennedy Musonda dakika ya 62.
Mabao mengine ya Nasry Kyombo (aliyejifunga) na Clement Mzize yalihakikisha ushindi wa Yanga na kufikisha jumla ya pointi 71 katikamsimamo wa ligi kuu 2023/2024, ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote ligi ikiwa imesalia na michezo michache kuisha.
Ushindi huu wa 30 unaiweka Yanga SC katika daraja la kipekee katika historia ya soka la Tanzania. Hakuna klabu nyingine iliyowahi kufikia mafanikio haya makubwa ususani katika ligi kuu ambayo ni ligi yenye ushindani mkubwa.
Ikumbukwe kua ushindi huu ni wa tatu mfululizo kwa Yanga, kuashiria uthabiti na ubora wa kikosi chao katika misimu ya hivi karibuni. Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi, aliwapongeza wachezaji wake kwa juhudi zao na kujituma licha ya upinzani mkali kutoka kwa Mtibwa Sugar. Gamondi, ambaye alichukua mikoba ya Nesreddine Nabi, ameendeleza utamaduni wa ushindi ndani ya klabu hiyo.
Mtibwa Sugar Yapambana Kuepuka Kushuka Daraja
Kwa upande mwingine, Mtibwa Sugar wanajikuta katika wakati mgumu wakihitaji kushinda mechi zao zote tatu zilizobaki ili kujinasua kutoka mkiani mwa ligi. Kocha wao, Zubeiry Katwila, alikiri kuwa makosa ya wachezaji wake yalisababisha kipigo hiki.
Yanga SC Kuwakilisha Tanzania Kombe la Klabubingwa Afrika (CAF Champions League)
Kama mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC wamepata nafasi ya kupeperusha bendera ya Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League). Hii ni fursa nyingine kwa klabu hiyo kuonyesha uwezo wao katika anga za kimataifa.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Mbappe Akubali Punguzo Kubwa la Mshahara Ili Kujiunga na Real Madrid
- Idadi ya Makombe Ya Yanga Ligi Kuu Tanzania
- Idadi ya Makombe ya Arsenal: Makombe ya Ligi Ya EPL, FA, na Zaidi
- Hizi Apa Takwimu za Stephane Aziz Ki na Feisal Salum 2023/2024
- Simba Sc Yafunga Safari Kuifata kagera Sugar (May 2024)
- Hiki Ndicho Kikosi Rasmi cha Brazil Copa America 2024
Weka Komenti