Siku 2 Zimesalia: Mwisho wa Kutuma Maombi Nafasi Za Kazi Jeshi la Polisi Ni 16/05/2024!

Siku 2 Zimesalia: Mwisho wa Kutuma Maombi Nafasi Za Kazi Jeshi la Polisi Ni 16/05/2024!

  • Je, ndoto yako ni kujiunga na Jeshi la Polisi Tanzania? Muda unayoyoma! Tarehe ya mwisho ya kutuma maombi ya nafasi za kazi za Polisi ni Alhamisi, tarehe 16 Mei 2024, na zimesalia siku 2 pekee.

Mwisho wa Kutuma Maombi Nafasi Za Kazi Jeshi la Polisi Ni 16/05/2024!

Mwisho wa Kutuma Maombi Nafasi Za Kazi Jeshi la Polisi Ni 16/05/2024!

Mnamo tarehe 9 Mei 2024, Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania alitangaza fursa mbalimbali za ajira kwa vijana wenye viwango tofauti vya elimu:

  • Shahada
  • Stashahada
  • Astashahada
  • Kidato cha Sita
  • Kidato cha Nne

Fursa hii ni ya kipekee kwa vijana wa Kitanzania wenye ari na sifa za kujiunga na kikosi cha ulinzi wa amani nchini Tanzania.

Sifa Za Muombaji Nafasi Za Kazi Polisi

Tangazo la ajira limeainisha sifa maalum kwa kila ngazi ya elimu. Hakikisha unaangalia kwa makini tangazo ili kujiridhisha kama una sifa zinazohitajika. Baadhi ya sifa za jumla ni pamoja na:

Uraia: Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.

Elimu:

  • Awe amehitimu kidato cha nne au sita kuanzia mwaka 2018 hadi 2023.
  • Waombaji wa kidato cha nne wawe na ufaulu wa daraja la kwanza hadi la nne (Division I – IV). Waombaji wenye ufaulu wa daraja la nne (Division IV) wawe na ufaulu wa alama (Point) 26 hadi 28.
  • Waombaji wa kidato cha sita wawe na ufaulu wa daraja la kwanza hadi la tatu (Division I – III).
  • Wahitimu wa Shahada na Stashahada wawe na umri kuanzia miaka 18 hadi 30 na wawe na fani zilizoainishwa kwenye tangazo.

Umri: Waombaji wa kidato cha nne na sita pamoja na wenye Astashahada wawe na umri kuanzia miaka 18 hadi 25.

Urefu: Awe na urefu usiopungua futi tano na inchi nane (5’8″) kwa wanaume, na futi tano inchi nne (5’4″) kwa wanawake.

Kitambulisho: Awe na kitambulisho cha taifa au namba ya utambulisho kutoka mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA).

Lugha: Awe na uwezo wa kuongea lugha ya Kiswahili na Kiingereza.

Afya: Awe na afya njema kimwili na kiakili iliyothibitishwa na daktari wa Serikali.

Hali ya Ndoa: Awe hajaoa/kuolewa au kuwa na mtoto.

Matumizi ya Dawa za Kulevya: Awe hajawahi kutumia dawa za kulevya.

Mafunzo: Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya taaluma ya Polisi.

Ajira ya Serikali: Awe hajaajiriwa au hajawahi kuajiriwa na taasisi nyingine ya Serikali.

Mahali pa Kazi: Awe tayari kufanya kazi za Polisi mahali popote Tanzania.

Gharama za Usaili: Awe tayari kujigharamia katika hatua zote za usaili endapo ataitwa kwenye usaili.

Alama za Mwilini: Asiwe na alama za kuchorwa mwilini (tattoo).

Kumbukumbu za Uhalifu: Asiwe na kumbukumbu za uhalifu.

Jinsi ya Kutuma Maombi Nafasi za Kazi Jeshi la Polisi

Mchakato wa kutuma maombi ni rahisi na unafanyika mtandaoni kupitia mfumo maalum wa ajira za polisi:

Andika barua yako ya maombi kwa mkono (handwriting) na ujumuishe namba zako za simu. Tuma barua hii kwa anuani ifuatayo:

  • Mkuu wa Jeshi la Polisi
  • S.L.P 961
  • DODOMA

Tuma maombi mtandaoni: Jaza fomu ya maombi mtandaoni kupitia mfumo wa Ajira wa Polisi: http://ajira.tpf.go.tz

Ajira Nyenginezo: Nafasi Mpya Za Kazi Chuo Kikuu cha SUA: Mwisho wa Kutuma Maombi ni 19 Mei 2024

Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo