Miloud Hamdi Ajiunga na Ismaily ya Misri Baada ya Kuipa Yanga Mataji 3

Miloud Hamdi Ajiunga na Ismaily ya Misri Baada ya Kuipa Yanga Mataji 3

Kocha wa zamani wa Yanga SC, Miloud Hamdi amejiunga na Ismaily SC ya Misri 🇪🇬 kwa mkataba wa mwaka mmoja. Kocha huyo mwenye uzoefu mkubwa katika soka la Afrika, anaanza ukurasa mpya akiwa na makocha wawili wasaidizi: Hammadi Saghier, Kocha Msaidizi kutoka Ubelgiji, na Marouane Silimani, Kocha wa Viungo kutoka Tunisia. Ismaily SC imemshawishi Hamdi kwa kumwongezea maradufu mshahara aliokuwa akipokea Yanga SC. Inatarajiwa kuwa klabu hiyo itamtangaza rasmi leo.

Safari ya Mafanikio ya Miloud Hamdi Akiwa Kocha Mkuu Yanga SC

Miloud Hamdi alijiunga na klabu ya Yanga SC katikati ya msimu uliopita, akitokea Singida Black Stars. Aliteuliwa kuchukua nafasi ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Sead Ramovic. Ndani ya muda mfupi wa kuinoa timu hiyo, aliiongoza Yanga SC kwenye mechi 12 za Ligi Kuu Tanzania Bara, akionyesha uwezo mkubwa wa kiufundi na mbinu sahihi za ushindi.

Miloud Hamdi Ajiunga na Ismaily ya Misri Baada ya Kuipa Yanga Mataji 3

Katika msimu huo mmoja pekee, Hamdi aliweka historia ya kuisaidia Yanga SC kutwaa mataji matatu makubwa. Mataji hayo ni:

  1. Kombe la Muungano,
  2. Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, na
  3. Kombe la Shirikisho la Azam (FA Cup).

Hatua hiyo ilimtambulisha zaidi kama kocha mwenye uwezo wa kuleta matokeo chanya kwa muda mfupi, jambo lililovutia klabu mbalimbali za Afrika, zikiwemo zile za Kaskazini mwa Bara hilo.

Hatua Mpya: Hamdi Atua Ismaily ya Misri

Baada ya mafanikio hayo ya kihistoria, Miloud Hamdi sasa anaanza ukurasa mpya na klabu ya Ismaily SC inayoshiriki Ligi Kuu ya Misri. Ismaily, klabu yenye historia ndefu katika soka la Misri na Afrika kwa ujumla, imempa Hamdi mkataba wa mwaka mmoja, ikiwa ni ishara ya imani waliyonayo kwa uwezo wake wa kiufundi.

Hamdi atakuwa na jukumu la kuirejesha Ismaily kwenye ubora wa ushindani, akisaidiwa na benchi lake la ufundi linaloundwa na wataalamu wawili kutoka Ubelgiji na Tunisia. Mbali na mkataba huo wa muda mfupi, taarifa kutoka kwa mtu wa karibu na meneja wa Hamdi zinaeleza kuwa klabu hiyo imemlipa mshahara mara mbili ya ule aliokuwa anapata Yanga SC.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Simba SC Yamalizana na Ayoub Lakred Huku Hatma ya Camara Ikiwa Gizani
  2. Makombe ya Yanga 2024/2025
  3. Timu zilizofuzu Robo Fainali Kombe la Dunia Vilabu 2025
  4. Chelsea Yamwaga Paundi Milioni 60 Kumsajili Mshambuliaji Joao Pedro
  5. Yanga SC Kusherehekea Vikombe 5 Leo Jijini Dar – Paredi Kubwa Yatarajiwa
  6. Messi Aondolewa Kombe la Dunia la Klabu Baada ya PSG Kuicharaza Inter Miami 4-0
  7. Yanga SC Yaibuka Bingwa wa Kombe la CRDB Baada ya Kuicharaza Singida BS 2-0
  8. Chelsea Yajipanga Kuzima Moto wa Di Maria Katika Mechi ya Usiku Dhidi ya Benfica
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo