Mwisho wa Kutuma Maombi ya Kazi JWTZ 2026
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetangaza nafasi za kuandikishwa jeshini kwa vijana wa Kitanzania kuanzia wahitimu wa kidato cha nne hadi vyuo vikuu. Mwisho wa Kutuma Maombi ya Kazi JWTZ 2026 umewekwa kuwa Aprili 28, 2026, ambapo maombi yatapokelewa kuanzia Aprili 15 hadi Aprili 28, 2026.
Tangazo hilo limetolewa na Luteni Kanali Kevin Byabato, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano.
Sifa za waombaji
Kwa mujibu wa tangazo hilo, waombaji wanapaswa kuwa raia wa kuzaliwa wa Tanzania na kuwa na afya nzuri, akili timamu na tabia njema. Pia hawapaswi kuwa na rekodi ya makosa ya jinai.
Wenye elimu ya kidato cha nne na sita wanapaswa kuwa na umri usiozidi miaka 25, huku wenye elimu ya juu wakitakiwa kuwa na umri usiozidi miaka 28.
Aidha, waombaji wanatakiwa kuwa na vyeti halisi vya kuzaliwa na vyeti vya elimu, na wasiwe wamewahi kuhudumu katika taasisi nyingine za ulinzi na usalama.
Utaratibu wa maombi
Maombi yanapaswa kuandikwa kwa mkono na kuwasilishwa Makao Makuu ya Jeshi Msalato, Dodoma. Waombaji wanapaswa kuambatanisha nakala ya kitambulisho cha Taifa au namba ya NIDA, cheti cha kuzaliwa, vyeti vya elimu na namba ya simu ya mkononi.
SOMA ZAIDI









Leave a Reply