Ratiba ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup 2025/2026
Droo ya hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB Federation Cup msimu wa 2025/2026 imekamilika Aprili 17, 2026 jijini Dar es Salaam, na kubainisha rasmi namna timu nane zitakavyokutana kuwania nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali. Ratiba hiyo imeleta mchanganyiko wa michezo mikubwa ikihusisha vilabu vyenye uzoefu pamoja na vinavyoonyesha ushindani mkubwa katika michuano hiyo.
Ratiba ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup 2025/2026 inaonesha kuwa mechi zote zitachezwa Mei 16 hadi 17, 2026 katika viwanja vilivyopangwa ndani ya Tanzania.
Ratiba Kamili ya Robo Fainali
Katika hatua ya robo fainali ya kombe la shirikisho la CRDB 2025/2026, mashabiki wataweza kushuhudia michezo minne
- Coastal Union VS Singida Black Stars
Uwanja: CCM Mkwakwani, Tanga - Simba SC VS TRA United
Uwanja: Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam - JKT Tanzania VS Yanga SC
Uwanja: Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam - Mashujaa FC VS Azam FC
Uwanja: Lake Tanganyika, Kigoma
Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo jijini Dar es Salaam unatarajiwa kuwa mwenyeji wa michezo miwili, hali inayoonyesha umuhimu wa jiji hilo katika hatua hii ya mashindano.
Muonekano wa Mchezo kwa Mchezo
Miongoni mwa michezo inayovutia macho ni pambano kati ya Simba SC dhidi ya TRA United, ambapo Simba wataingia wakiwa na lengo la kusonga mbele huku TRA United wakisaka nafasi ya kufanya matokeo chanya.
Katika mchezo mwingine, JKT Tanzania watakutana na Yanga SC, pambano linalotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na uzito wa timu hizo katika soka la ndani.
Kwa upande wa Tanga, Coastal Union watawakaribisha Singida Black Stars katika Uwanja wa CCM Mkwakwani, wakati Mashujaa FC watamenyana na Azam FC katika Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.
Michezo ya Nusu Fainali
Kwa mujibu wa mpangilio wa mashindano, washindi wa robo fainali wataingia hatua ya nusu fainali kwa mfumo ufuatao:
- Simba SC / TRA United 🆚 Coastal Union / Singida Black Stars
- Mashujaa FC / Azam FC 🆚 JKT Tanzania / Yanga SC
Mapenedekezo ya Mhariri:








Leave a Reply