Nafasi Mpya za Kazi Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania Agosti 2024
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kimetangaza nafasi mpya za kazi kwa fani mbalimbali za taluma mwezi Agosti 2024. Chuo hiki ni taasisi ya umma iliyoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Na. 17 ya mwaka 1992. Tangu tarehe 1 Januari, 2007, chuo kimekuwa kikifanya kazi chini ya hati ya OUT-Charter Inc. ya mwaka 2007, ambayo inaendana na Sheria ya Vyuo Vikuu Na. 7 ya mwaka 2005.
Dira na Dhamira ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kinafanya kazi kwa kufuata dira ya kutoa elimu bora, inayofaa, rahisi kufikiwa, na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa elimu huria na elimu ya mtandao (online). Pia, chuo kinafanya tafiti na kutoa huduma kwa jamii ili kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini Tanzania na ulimwenguni kote.
OUT ina makao makuu yake Kinondoni, Dar es Salaam, pamoja na vituo vya mikoa 30 nchini Tanzania Bara, ikiwemo vituo vya uratibu vya visiwani Zanzibar – Unguja na Pemba.
Nafasi za Kazi Zinazotangazwa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kinakaribisha maombi kutoka kwa watanzania wenye sifa na uwezo stahiki kwa nafasi zifuatazo:
- Tutorial Assistant (Education And Entrepreneurship) – Nafasi 1
- Tutorial Assistant (Law) – Nafasi 2
- Tutorial Assistant (Human Resource Management) – Nafasi 1
- Tutorial Assistant (Botany) – Nafasi 1
- Tutorial Assistant (Law) – Nafasi 1 (Imetangazwa tena)
- Tutorial Assistant (Finance) – Nafasi 1 (Imetangazwa tena)
- Assistant Lecturer (Special And Inclusive Education) – Nafasi 1
- Assistant Lecturer (Early Childhood Education And Development) – Nafasi 1
- Assistant (Marketing) – Nafasi 1
- Assistant Lecturer (Accounting) – Nafasi 1
- Assistant Lecturer (Mathematics) – Nafasi 1
- Assistant Lecturer (English/Linguistics) – Nafasi 1
- Assistant Lecturer (Social Work) – Nafasi 1
- Assistant Lecturer (Development Studies) – Nafasi 1
Masharti ya Jumla kwa Waombaji
- Mwombaji lazima awe raia wa Tanzania mwenye umri usiozidi miaka 45.
- Waombaji wanatakiwa kuambatisha wasifu wao (CV) uliosheheni taarifa za uhakika kama vile anuani, namba za simu, na barua pepe.
Maombi yote yanapaswa kuzingatia taarifa zilizotangazwa kwenye tangazo hili la ajira. - Waombaji wanapaswa kuambatisha nakala za vyeti vilivyothibitishwa ikiwa ni pamoja na cheti cha kuzaliwa, vyeti vya elimu ya juu, diploma, au vyeti vya mafunzo mengine.
- Matokeo ya mitihani na hati za matokeo ya kidato cha nne na sita hazitakubalika kama vielelezo.
- Mwombaji anatakiwa kupakia picha ndogo ya pasipoti kwenye mfumo wa kuomba kazi.
- Wafanyakazi wa umma lazima wapitishe maombi yao kwa waajiri wao wa sasa.
- Wastaafu wa utumishi wa umma hawapaswi kuomba.
- Waombaji wanatakiwa kuwasilisha majina ya watu watatu wa rufaa wenye mawasiliano ya uhakika.
- Vyeti kutoka vyuo vya nje ya nchi lazima viidhinishwe na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) au Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).
- Mwombaji mwenye mahitaji maalum (ulemavu) anashauriwa kueleza hali yake.
- Barua ya maombi iwekwe saini na mwombaji, iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza, na ipelekwe kwa: Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Mipango, Fedha, na Utawala), Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, S.L.P 23409 Dar Es Salaam.
- Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 26 Agosti 2024.
- Waombaji watakaochaguliwa kwa ajili ya usaili watajulishwa tarehe ya usaili.
- Uwasilishaji wa vyeti vya kughushi utasababisha hatua za kisheria kuchukuliwa.
Jinsi ya Kutuma Maombi
Maombi yote ya kazi lazima kwa nafasi zilizotangazwa na chuo kikuu huria cha Tanzania yanatakiwa kuwasilishwa kupitia Mfumo wa Ajira Mtandao kwa kutumia anwani ifuatayo: http://portal.ajira.go.tz na si vinginevyo. Anuani hii pia inaweza kupatikana kwenye Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Nafasi Mpya Za Kazi Shirika La Bima ya Taifa (NIC) 11-08-2024
- Nafasi Mpya za Kazi Taasisi Mbalimbali za Umma: 11-08-2024
- Nafasi Mpya Za Kazi MDAs NA LGAs Agosti 2024
- Mfano wa Barua Ya Maombi ya Kazi MDAs NA LGAs
- Nafasi za Kazi JWTZ 2024 (Ajira Jeshi la wananchi Tanzania)
- Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)
- Nafasi Mpya za Kazi Chuo Kikuu Cha Sokoine SUA Agosti 2024
Weka Komenti