Nafasi Mpya za Kazi Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi Novemba 2024
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi Ishirini na nane (28) zilizotangazwa rasmi mwezi Novemba 2024.
Nafasi hizi zinajumuisha nafasi za Mkaguzi Daraja la II katika fani mbalimbali, zikiwa na lengo la kuimarisha usimamizi wa matumizi ya rasilimali za umma kwa kuzingatia Sheria na Kanuni za Serikali.
Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi ni taasisi inayotekeleza majukumu ya kikatiba ya kudhibiti fedha za Serikali na kuhakikisha matumizi sahihi ya rasilimali za umma. Kwa mujibu wa Sheria ya Ukaguzi wa Umma, sura ya 418, ofisi hii ina jukumu la kukagua mapato na matumizi ya rasilimali za umma ili kuhakikisha uwazi na uwajibikaji. Waombaji wanaopenda kujiunga na nafasi hizi wanahitajika kutuma maombi yao kupitia mfumo wa kielektroniki wa Ajira kabla ya tarehe 26 Novemba 2024.
Nafasi Mpya za Kazi Zilizotangazwa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi
1. Mkaguzi Daraja la II (Ukaguzi wa Hesabu) – Nafasi 21
Wajibu wa mkaguzi katika nafasi hii ni pamoja na kushiriki katika uandaaji wa mpango wa ukaguzi, kukagua nyaraka za matumizi na miradi ya serikali, na kutayarisha ripoti za ukaguzi. Waombaji wanapaswa kuwa na Shahada ya kwanza ya Uhasibu na Mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
2. Mkaguzi Daraja la II (Ukaguzi wa Mifumo ya Taarifa – Fani ya Usalama wa Mifumo ya TEHAMA) – Nafasi 3
Mkaguzi atakayejaza nafasi hii atashughulika na ukaguzi wa mifumo ya habari yenye lengo la kuboresha usalama na ufanisi. Waombaji wana sifa za Shahada katika Usalama wa Mtandao, Usalama wa Mifumo ya TEHAMA, au Usalama wa Mtandao wa Kompyuta kutoka vyuo vinavyotambuliwa.
3. Mkaguzi Daraja la II (Ukaguzi wa Ufanisi – Fani ya Sayansi ya Siasa) – Nafasi 2
Nafasi hii inalenga kufanya tathmini ya ufanisi wa programu na sera mbalimbali za serikali. Majukumu ya nafasi hii ni pamoja na kuandaa ripoti na mipango ya kazi. Waombaji wenye Shahada ya Sayansi ya Siasa na Utawala au Sayansi ya Siasa wanahamasishwa kuomba.
4. Mkaguzi Daraja la II (Ukaguzi wa Kiuchunguzi – Fani ya Usalama wa Mifumo ya TEHAMA) – Nafasi 1
Mkaguzi katika nafasi hii anahitajika kuwa na ujuzi maalum wa kuchambua taarifa na kufanya ukaguzi wa kina kwa lengo la kuhakikisha uadilifu na usalama wa mifumo. Waombaji wanatakiwa kuwa na Shahada katika Usalama wa Mtandao, Sayansi ya Kompyuta, au Uhandisi wa Kompyuta na pia vyeti vya kitaaluma kama Certified Ethical Hacker (CEH) au Cisco Certified Network Associate in Security (CCNA).
5. Mkaguzi Daraja la II (Ukaguzi wa Kiuchunguzi – Fani ya Utengenezaji wa Programu za TEHAMA) – Nafasi 1
Kwa waombaji wenye utaalamu wa kutengeneza programu, nafasi hii inatoa fursa ya kushiriki katika ukaguzi wa mifumo na programu. Majukumu ni pamoja na kuandaa mipango ya ukaguzi wa kiuchunguzi na kuchanganua ushahidi wa mifumo. Shahada katika Sayansi ya Kompyuta, Uhandisi wa Programu, au Teknolojia ya Habari ni sifa muhimu kwa nafasi hii.
Masharti ya Jumla kwa Waombaji
Waombaji wote wanapaswa kuwa na sifa zifuatazo:
- Uraia: Awe raia wa Tanzania mwenye umri usiozidi miaka 45, isipokuwa kwa walioko kazini Serikalini.
- Maombi: Maombi yote yawasilishwe kupitia mfumo wa kielektroniki wa Ajira kupitia anuani ya http://portal.ajira.go.tz/.
- Nyaraka Muhimu: Maombi yaambatane na vyeti halisi vilivyothibitishwa, ikiwa ni pamoja na cheti cha kuzaliwa na vyeti vya taaluma.
- Uthibitisho wa Vyeti: Waombaji waliopata elimu nje ya Tanzania wanapaswa kuhakikisha vyeti vyao vimethibitishwa na TCU, NECTA, au NACTE.
- Tarehe ya Mwisho ya Kutuma Maombi: Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 26 Novemba, 2024. Maombi yatakayowasilishwa nje ya mfumo wa kielektroniki wa Ajira hayatapokelewa.
Jinsi ya Kutuma Maombi ya Kazi Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi
Maombi yote yanapaswa kuwasilishwa kupitia mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kwa anuani https://portal.ajira.go.tz/ kabla ya tarehe 26 Novemba 2024. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu uliowekwa HAYATAFIKIRIWA.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Simba Queens yaendeleza ubabe Soka la Wanawake
- Ratiba ya Mechi za Leo 14/11/2024
- Nafasi 3 za Kazi ya Dereva Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi | Mwisho 06 November 2024
- Majina ya Walioitwa kwenye Usaili Ajira za Walimu 2024 MDAs & LGAs
- Majina Ya Walimu Walioitwa Kwenye Usaili 2024
- Nafasi Za Kazi Baraza La Mitihani Tanzania NECTA – October 2024
- Nafasi 10 Za Kazi Msaidizi Maendeleo Ya Jamii Halmashauri Ya Wilaya Ya Kyela
Leave a Reply