Nafasi Mpya za Kazi Ualimu MDAs NA LGAs 17-09-2024

Nafasi Mpya za Kazi Ualimu MDAs NA LGAs 17-09-2024 | Ajira Mpya za Walimu MDAs NA LGAs September 2024

Sekta ya elimu inazidi kuimarishwa nchini Tanzania, na hivi leo septema 17 2024 karibuni Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ametangaza nafasi mpya za kazi kwa waalimu katika Sekretarieti za Mikoa (MDAs) na Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGAs).

Tangazo hili linatoa fursa kwa Watanzania wenye sifa stahiki kuomba nafasi hizi zinazohusu masomo mbalimbali ya ufundi na teknolojia, ambazo zina lengo la kuboresha viwango vya elimu ya ufundi katika shule za sekondari na vyuo vya ufundi. Hii ni fursa adhimu kwa wale walio na ujuzi katika taaluma husika na walio tayari kuchangia kwenye maendeleo ya sekta ya elimu nchini.

Nafasi Mpya za Kazi Ualimu MDAs NA LGAs 17-09-2024

Nafasi Mpya za Kazi Ualimu MDAs NA LGAs 17-09-2024

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ametangaza jumla ya nafasi 600 za ualimu, ambazo zimegawanywa katika masomo tofauti kulingana na ujuzi maalum wa ufundi na teknolojia. Zifuatazo ni nafasi mpya za kazi ya Ualimu zilizotangazwa:

  1. Mwalimu Daraja La III B – Somo La Ushonaji (Designing, Sewing And Cloth Technology) Nafasi 17
  2. Mwalimu Daraja La III B – Somo La Uashi (Masonry And Bricklaying) Nafasi 26
  3. Mwalimu Daraja La III B – Somo La Ufundi Wa Bomba (Plumbing And Pipe Fitting) Nafasi 18
  4. Mwalimu Daraja La III B – Somo La Uselemala (Carpentry And Joinery With Metal Works) Nafasi 18
  5. Mwalimu Daraja La III B – Somo La Upakaji Rangi Na Uandikaji Maandishi (Painting And Sign Writing) Nafasi 3
  6. Mwalimu Daraja La III B – Somo La Upoaji Na Viyeo Vya Hewa (Refrigeration And Air Conditioning) Nafasi 9
  7. Mwalimu Daraja La III B – Somo La Michezo (Sports General) Nafasi 2
  8. Mwalimu Daraja La III B – Somo La Usindikaji Wa Mbao (Wood Processing) Nafasi 5
  9. Mwalimu Daraja La III B – Somo La Uzalishaji Wa Chakula (Food Production) Nafasi 08
  10. Mwalimu Daraja La III B – Somo La Umeme Wa Magari (Auto Electrical) Nafasi 85
  11. Mwalimu Daraja La III B – Somo La Ulehemu Na Utengenezaji Wa Vyuma (Welding And Metal Fabrication) Nafasi 20
  12. Mwalimu Daraja La III B – Somo La Ufundi Wa Magari (Motor Vehicle Mechanics) Nafasi 20
  13. Mwalimu Daraja La III B – Somo La Chakula Na Vinywaji, Mauzo Na Huduma (Food And Bevarage, Sales And Services) Nafasi 05
  14. Mwalimu Daraja La III C – Somo La Ufungaji Umeme (Electrical Installation) Nafasi 20
  15. Mwalimu Daraja La III C – Somo La Michezo (Sports And Games) Nafasi 08
  16. Mwalimu Daraja La III C – Somo La Utengenezaji Programu Za Tehama (Computer Programming) Nafasi 16
  17. Mwalimu Daraja La III C – Somo La Sanaa Ya Uigizaji Na Utumbuizaji Wa Muziki (Theather Arts And Music Perfomance) Nafasi 08
  18. Mwalimu Daraja La III C – Somo La Ufungaji Wa Nishati Ya Jua (Solar Power Installation) Nafasi 15
  19. Mwalimu Daraja La III C – Somo La Afya Ya Wanyama Na Uzalishaji (Animal Health Production) Nafasi 10
  20. Mwalimu Daraja La III C – Somo La Uzalishaji Wa Kilimo Cha Bustani (Horticulture Production) Nafasi 07
  21. Mwalimu Daraja La III C – Somo La Uzalishaji Wa Mazao (Crop Production) Nafasi 20
  22. Mwalimu Daraja La III C – Somo La Uvuvi Na Usindikaji Wa Samaki (Fishing And Fish Processing) Nafasi 10
  23. Mwalimu Daraja La III B – Somo La Biashara (Commerce) Nafasi 125
  24. Mwalimu Daraja La III B – Somo La Biashara (Bookkeeping) Nafasi 125

Vigezo na Masharti kwa Waombaji Nafasi Mpya za Kazi Ualimu MDAs NA LGAs

Waombaji wanatakiwa kuzingatia masharti yafuatayo:

  • Raia wa Tanzania: Waombaji lazima wawe na uraia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45, isipokuwa kwa waajiriwa wa serikali.
  • Sifa za Kielimu: Waombaji wote waambatishe Hati ya Matokeo (Academic Transcript) pamoja na vyeti vya taaluma vinavyolingana na nafasi wanayoomba. Vyeti vya kidato cha nne, sita, diploma au shahada vitahitajika kulingana na nafasi.
  • Waombaji wenye ulemavu: Wanahamasishwa kuomba, na wanapaswa kueleza aina ya ulemavu walionao katika mfumo wa maombi.
    Cheti cha kuzaliwa: Waombaji lazima waambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na wakili.
  • Waombaji waliopo kazini: Wale walioko kwenye Utumishi wa Umma wanapaswa kuwasilisha maombi yao kupitia kwa waajiri wao.

Jinsi ya Kutuma Maombi Nafasi Mpya za Kazi Ualimu MDAs NA LGAs 17-09-2024

Maombi ya kazi yanapaswa kuwasilishwa kupitia mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kwa anuani ya tovuti ifuatayo: http://portal.ajira.go.tz.

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 30 Septemba, 2024. Waombaji wanapaswa kuambatisha barua ya maombi iliyosainiwa, pamoja na vyeti vyao vya elimu na maelezo binafsi (C.V) yenye anwani za kuaminika za wadhamini watatu.

Waombaji wanapaswa kuambatisha barua ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;

  • KATIBU,
  • OFISI YA RAIS,
  • SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
  • S.L. P. 2320, DODOMA.

Fursa za Kipekee kwa Waombaji

Hii ni fursa ya kipekee kwa waombaji wenye ujuzi wa ufundi na teknolojia kuchangia kwenye maendeleo ya sekta ya elimu nchini Tanzania. Kufundisha masomo ya ufundi kama vile uselemala, umeme, ushonaji na teknolojia ya mavazi, ni muhimu katika kukuza ujuzi wa wanafunzi na kuwajengea uwezo wa kujiajiri au kupata ajira kwenye sekta mbalimbali.

Kwa waombaji wenye ulemavu, kuna fursa maalum ya kuomba nafasi hizi, jambo ambalo linaonesha kujali na kuzingatia usawa katika ajira. Pia, kwa vijana wenye elimu ya ufundi, nafasi hizi zinatoa nafasi ya kutumia ujuzi walioupata na kuufundisha kwa vizazi vijavyo.

Bofya Hapa Kupakua Tangazo La Ajira Mpya za Walimu MDAs NA LGAs

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Taarifa Muhimu kwa Waombaji Kazi za Ualimu AJira Portal 14 September 2024
  2. Kuhakiki Mwajiri Ajira Portal (Employer Confirmation): Mwongozo Kamili kwa Walimu
  3. Majina ya Walioitwa kwenye Usaili Ajira Portal 2024
  4. Jinsi ya Kubadili Kituo Cha Usaili Ajira Portal
  5. Viwango Vipya vya Posho Serikalini 2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo