Nafasi Za Kazi Afisa Uchunguzi Takukuru April 2026
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imetangaza rasmi nafasi mpya 250 za ajira kwa nafasi ya Afisa Uchunguzi kwa Watanzania wenye sifa stahiki, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha utendaji wa taasisi hiyo katika ngazi ya wilaya kote Tanzania Bara.
Tangazo hilo, lililochapishwa tarehe 11 Aprili 2026 na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, linatoa fursa kwa wataalamu na wahitimu wa kada mbalimbali kujiunga na taasisi inayosimamia mapambano dhidi ya rushwa nchini. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, jumla ya nafasi 500 zimetangazwa, zikigawanywa katika kada mbili kuu: Afisa Uchunguzi na Mchunguzi Msaidizi.
Sifa za Waombaji wa Kazi ya Afisa Uchunguzi TAKUKURU (Nafasi 250)
Kwa nafasi ya Afisa Uchunguzi, waombaji wanatakiwa kuwa na shahada ya kwanza kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali katika fani mbalimbali, zikiwemo:
- Uhasibu
- Usimamizi wa Biashara
- Uhandisi (Ujenzi, Umeme, Mitambo, Mafuta na Gesi)
- Sayansi ya Kompyuta / TEHAMA
- Uchumi na Mipango
- Sheria
- Lishe na Sayansi ya Chakula
- Usimamizi wa Rasilimali Watu
- Ununuzi na Ugavi
- Takwimu
Na fani nyingine zilizoainishwa kwenye tangazo
Waombaji wanapaswa kuwa na ufaulu wa kuanzia daraja la pili la chini (Lower Second Class), huku waliosajiliwa na bodi za kitaaluma wakipewa kipaumbele.
Aidha, mwombaji hatakiwi kuzidi umri wa miaka 29 ifikapo Mei 2026.
Masharti ya Jumla kwa Waombaji
TAKUKURU imeweka masharti ya jumla yanayopaswa kuzingatiwa na waombaji wote, yakiwemo:
- Kuwa na uadilifu wa hali ya juu
- Kutokuwa na rekodi ya uhalifu
- Kuwa tayari kufanya kazi katika wilaya yoyote Tanzania Bara
- Kutowahi kufukuzwa au kuachishwa kazi katika utumishi wa umma
Waombaji wanatakiwa kuwasilisha nyaraka muhimu zikiwemo vyeti vya elimu, cheti cha kuzaliwa, wasifu binafsi (CV), pamoja na mawasiliano ya wadhamini watatu. Aidha, namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) ni ya lazima.
TAKUKURU imeonya kuwa:
“Mwombaji atakayewasilisha vyeti vya kughushi au kutoa taarifa za uongo atachukuliwa hatua za kisheria.”
Vyeti vya elimu kutoka nje ya nchi vinapaswa kuthibitishwa na mamlaka husika nchini kama TCU, NACTVET au NECTA.
Utaratibu wa Kutuma Maombi
Maombi yote yanapaswa kuwasilishwa kupitia mfumo rasmi wa ajira wa TAKUKURU kwa njia ya mtandao:
Kwa mujibu wa tangazo, maombi yatakayowasilishwa kwa njia ya posta au kwa mkono hayatapokelewa.
Barua za maombi zinapaswa kuelekezwa kwa:
- Mkurugenzi Mkuu,
- Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU),
- Mtaa wa Jamhuri,
- S.L.P. 1291,
- 1101 Dodoma
Mwisho wa Kutuma Maombi
Mwisho wa kuwasilisha maombi ni tarehe 03 Mei 2026.
Waombaji watakaokidhi vigezo na kupita hatua ya awali ya uchambuzi ndio watakaowasiliana kwa hatua zinazofuata za mchakato wa ajira.
Mapendekezo ya Mhariri:









Leave a Reply