Majina ya walioitwa kwenye Usaili Tume ya Utumishi wa Mahakama JSC

Majina ya walioitwa kwenye Usaili Tume ya Utumishi wa Mahakama JSC

Tume ya Utumishi wa Mahakama (JSC) imetoa orodha ya majina ya waombaji waliofanikiwa kuingia katika hatua ya kwanza ya usaili kwa nafasi mbalimbali za kazi. Tangazo hili linafuatia tangazo la awali la nafasi za ajira lililotolewa tarehe 5 Julai, 2024.

Waombaji wote waliotuma maombi ya kazi wanatakiwa kuangalia kama majina yao yapo katika pdf dokumenti yenye orodha ya majina ya walioitwa kwenye usaili tume ya utumishi wa mahakama JSC ambayo tumeiambatanisha mwishoni mwa chapisho hili. Pia waliofanikiwa kuchaguliwa kwa ajili ya usaili wanatakiwa kuwa makini na kufuatilia hatua za usaili zilizopangwa na tume. Usaili huu ni sehemu muhimu katika mchakato wa kupata nafasi za ajira katika kada mbalimbali zilizotangazwa na jsc.

Majina ya walioitwa kwenye Usaili Tume ya Utumishi wa Mahakama JSC

Tarehe na Utaratibu wa Usaili Tume ya Utumishi wa Mahakama JSC

Usaili wa awali utafanyika kwa njia ya kielektroniki kwa kada zote zilizoainishwa. Kila kada imepewa tarehe maalum za usaili ambazo zitaanza kuanzia saa 2:30 asubuhi. Waombaji wote waliochaguliwa kwa ajili ya usaili wa awali wanashauriwa kuhakikisha kuwa wanatambua tarehe na wakati wa usaili wao ili kuepuka matatizo yoyote.

Kwa wale ambao watafaulu usaili wa awali, watafahamishwa kuhusu tarehe za usaili wa pili ambao unatarajiwa kua wa maojiano. Usaili wa ziada utajumuisha usaili wa kujieleza (Oral Interview) na/au usaili wa vitendo (Practical Interview). Taarifa hizi zitatolewa kupitia tovuti rasmi ya Tume ya Utumishi wa Mahakama: www.jsc.go.tz.

Kuangalia Majina ya walioitwa kwenye Usaili Tume ya Utumishi wa Mahakama JSC

Ili kuangalia majina ya walioitwa kwenye usaili wa Tume ya Utumishi wa Mahakama (JSC), waombaji wa nafasi za ajira wanashauriwa kutembelea tovuti rasmi ya Tume: www.jsc.go.tz. Orodha kamili ya majina ya waombaji waliochaguliwa inapatikana kwenye tovuti hiyo, ambapo waombaji wanapaswa kuangalia majina yao pamoja na vituo na muda uliopangwa kwa usaili.

Kwa urahisi zaidi, tumekuandalia kiungo cha moja kwa moja hapa chini ambacho kitakupeleka kwenye PDF rasmi yenye majina ya walioitwa kwenye usaili pamoja na maelezo yote muhimu kuhusu mchakato wa usaili wa JSC.

Pata Orodha ya Majina na Maelezo ya Usaili Hapa

Mapendekezo ya mhariri:

  1. Nafasi Mpya za Kazi Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania Agosti 2024
  2. Nafasi Mpya Za Kazi Shirika La Bima ya Taifa (NIC) 11-08-2024
  3. Nafasi Mpya za Kazi Taasisi Mbalimbali za Umma: 11-08-2024
  4. Nafasi Mpya Za Kazi MDAs NA LGAs Agosti 2024
  5. Mfano wa Barua Ya Maombi ya Kazi MDAs NA LGAs
  6. Nafasi za Kazi JWTZ 2024 (Ajira Jeshi la wananchi Tanzania)
  7. Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo