Nauli ya Treni ya Umeme ya SGR Dar to Dodoma | Bei ya Tiketi za Treni ya Umeme Dar es salaam to Dodoma
Safari ya treni ya mwendokasi katika reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma sasa zimeanza rasmi. Treni hii ya umeme, inayojulikana kwa jina la “express train,” inatoa huduma za kisasa na za haraka, ikiwa ni hatua kubwa katika kuboresha miundombinu ya usafiri nchini Tanzania. Hii ni habari njema kwa wasafiri kwani sasa wanaweza kufika Dodoma kwa muda mfupi zaidi, huku wakifurahia huduma za kipekee ndani ya treni.
Ratiba ya Safari na Vituo Treni ya Umeme ya SGR Dar to Dodoma
Treni ya Umeme ya SGR imeanza safari zake za Dar kwenda Dodoma rasmi Julai 25, 2024. Treni hii inaanza safari Dar es Salaam saa 12:00 asubuhi na kufika Dodoma saa 3:25 usiku, ikimaanisha safari nzima itachukua saa tatu na dakika 25 pekee. Treni hii itasimama Morogoro pekee kabla ya kuendelea na safari hadi Dodoma. Kwa wale wanaosafiri na treni ya kawaida, safari itaanza saa 3:30 asubuhi kutoka Dar es Salaam na kufika Dodoma baada ya kusimama katika vituo vidogo kama vile Pugu.
Nauli ya Treni ya Umeme ya SGR Dar to Dodoma
Nauli za treni ya SGR zinatofautiana kulingana na aina ya treni na daraja la huduma unalochagua:
Treni ya Kawaida
Nauli ni Tsh 31,000 kwa safari ya kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma.
Treni ya Haraka (Express Train)
- Daraja la Biashara (Business Class): Tsh 70,000
- Daraja la Juu (Royal Class): Tsh 120,000
Upatikanaji wa Tiketi za Treni ya Umeme ya SGR Dar to Dodoma
Tiketi za treni zote zinapatikana kwa njia ya mtandao (online) kupitia tovuti rasmi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) na pia katika stesheni za SGR. Kwa muongozo kamili wa kukata tiketi mtandaoni tafadhali angalia chapisho letu hapa, Jinsi Ya kukata Tiketi Ya Treni Online. Hii inawezesha wasafiri kufanya maandalizi ya safari kwa urahisi na kwa wakati wao, huku wakihakikisha wanapata tiketi mapema.
Mapendekezo ya Mhariri:
Kuwekwe na ratiba ya mchana Dar Dodoma maana tunakaa mbali kuwahu hiyo saa 12.00 tutashindwa ikizingatiwa vituo vya njiani haisimami
Nauli zenu ni kukomoa raia ilifaa kwamba kue na bei ambayo mtu yoyote ata mwenye uwezo wa chini kabsa aweze kuitumia lkn kukiwa na hiyo hali ya kwamba mfanya biashara mwenye 70k hadi120k ndio anatumia vipi hawa wa chini zaidi inamaana wao sio kwaajili yao ??