Orodha ya Vijana 3500 Waliochaguliwa Kujiunga Jeshi la Polisi Tanzania 2024 Yatangazwa

Orodha ya Vijana 3500 Waliochaguliwa Kujiunga Jeshi la Polisi Tanzania 2024 Yatangazwa

Jeshi la Polisi nchini Tanzania limetangaza rasmi orodha ya vijana 3,500 waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Polisi kwa mwaka 2024. Taarifa hiyo, iliyotolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillius M. Wambura, mnamo Septemba 23, 2024, imeeleza kuwa vijana hao wanapaswa kuripoti kwa mafunzo ya awali kuanzia Septemba 30 hadi Oktoba 2, 2024 katika Shule ya Polisi Moshi.

Katika taarifa hiyo, IGP Wambura amesisitiza umuhimu wa kuripoti kwa wakati na kuzingatia maelekezo yote yaliyotolewa ili kuhakikisha mafunzo yanaanza kwa utaratibu uliopangwa.

“Vijana waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti katika Shule ya Polisi Moshi kwa tarehe zilizotajwa, na yeyote atakayeshindwa kufika kwa muda uliopangwa atahesabika kama amejiondoa kwenye mafunzo hayo,” ilisisitiza taarifa hiyo.

Utaratibu wa Kuripoti kwa Vijana Waliochaguliwa Kujiunga Jeshi la Polisi Tanzania 2024

Waliopitia Usaili wa Dar es Salaam na Vikosi Vilivyo Chini ya Makao Makuu ya Polisi

Vijana waliofanyiwa usaili katika Chuo cha Taaluma ya Polisi (DPA) Dar es Salaam na vikosi vilivyo chini ya Makao Makuu ya Jeshi la Polisi wanatakiwa kuripoti kwenye Barracks ya Polisi, Barabara ya Kilwa, karibu na Hospitali Kuu ya Polisi mnamo Septemba 30, 2024 saa 12:00 asubuhi. Kutoka hapo, watasafirishwa moja kwa moja hadi Shule ya Polisi Moshi kwa ajili ya mafunzo.

Vijana Waliofanyiwa Usaili Mikoa ya Bara

Kwa vijana waliofanyiwa usaili kwenye mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara, wanatakiwa kuripoti kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa husika mnamo Septemba 29, 2024 saa 2:00 asubuhi kwa ajili ya kupewa maelekezo ya safari yao ya kwenda Shule ya Polisi Moshi.

Vijana Waliofanyiwa Usaili Zanzibar (Unguja na Pemba)

Vijana waliopitia usaili katika visiwa vya Unguja na Pemba, wanatakiwa kuripoti Makao Makuu ya Polisi Zanzibar (Ziwani) mnamo Septemba 29, 2024 kwa ajili ya kupangwa utaratibu wa safari yao.

Vifaa Muhimu vya Kujitayarisha Navyo

Kabla ya kuanza mafunzo yao rasmi, vijana wote wanatakiwa kuripoti wakiwa na vifaa mbalimbali muhimu kwa ajili ya mafunzo. Orodha ya vifaa hivi ni pamoja na:

  1. Track suit ya rangi ya bluu yenye ufito mweupe, fulana nyeupe isiyo na maandishi, na raba.
  2. Vifaa vya usafi kama vile reki, jembe lenye mpini, panga, ndoo mbili ndogo, na fagio la chelewa.
  3. Chandarua cha duara, shuka za rangi ya light blue, na blanket la kijivu.
  4. Vyeti vya taaluma pamoja na nakala za vyeti hivyo, kadi ya NIDA au namba ya utambulisho wa taifa, na pasipoti ndogo sita za rangi ya samawati (blue).
  5. Fedha za kujikimu pamoja na kadi ya Bima ya Afya (NHIF), au Tsh. 50,400/= kwa wasio na kadi za bima.

Maelekezo Muhimu kwa Waliochaguliwa Kujiunga Jeshi la Polisi

Jeshi la Polisi pia limeweka sheria madhubuti kwa vijana wote watakaohudhuria mafunzo. Miongoni mwa sheria hizo ni marufuku ya kubeba simu za mkononi. Simu yoyote itakayokamatwa chuoni itachukuliwa kama utovu wa nidhamu na mhusika atafukuzwa mafunzo mara moja. Viongozi wa shule watatoa utaratibu wa mawasiliano rasmi kwa wanafunzi.

Aidha, vijana wanaotarajia kuripoti baada ya tarehe 02/10/2024 hawatapokelewa na watatambulika kuwa wamejiondoa kwenye mafunzo. Hivyo, ni muhimu kwa vijana waliochaguliwa kujiunga na Jeshi la Polisi kuhakikisha wanazingatia tarehe na maelekezo yote yaliyoainishwa.

Hitimisho: Orodha kamili ya vijana 3,500 waliochaguliwa kujiunga na Jeshi la Polisi Tanzania 2024 imetolewa rasmi na inaweza kupatikana kupitia tovuti ya Jeshi la Polisi au mwishoni mwa champisho hili. Jeshi la Polisi linawahimiza vijana waliopata nafasi hiyo adhimu kuzingatia maelekezo yote na kuhakikisha wanaripoti kwa wakati ili kuanza safari yao ya kitaaluma na kiaskari.

Angalia Majina ya Vijana 3500 Waliochaguliwa Kujiunga Jeshi la Polisi Tanzania 2024 Kupitia PDF hii apa chini

TANGAZO-LA-KURIPOTI-SHULE-YA-POLISI-MOSHI

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga na Jeshi la Polisi 2024
  2. Majina ya Walioitwa kwenye Usaili Ajira Portal 2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo