Ratiba ya Kombe la Muungano Leo 23/04/2026
Michuano ya robo fainali ya Kombe la Muungano inaendelea leo kwa mechi mbili muhimu zinazotarajiwa kukamilisha hatua hii ya mashindano, huku timu nne zikipambana kuwania nafasi ya kutinga nusu fainali.
Kwa mujibu wa ratiba rasmi ya leo Alhamisi, Aprili 23, 2026, michezo yote itapigwa katika dimba la New Amaan Complex, Zanzibar, ambapo mashabiki wanatarajia kushuhudia ushindani mkali katika kila dakika ya mchezo.
Mechi za Leo Robo Fainali Muungango Cup 2026
Katika mchezo wa mapema utakaochezwa saa 10:15 jioni, Mlandege FC watakutana na Singida BS SC katika pambano linalotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na hamasa ya kufuzu hatua inayofuata.
Baadaye usiku, saa 2:15, Simba SC wataingia uwanjani dhidi ya Mafunzo SC katika mchezo mwingine wa kusisimua wa kukamilisha ratiba ya robo fainali.
Nani Atafuzu Nusu Fainali?
Kwa mujibu wa mfumo wa mashindano, washindi wa mechi hizi mbili za leo watafanikiwa kufuzu moja kwa moja hatua ya nusu fainali ya Kombe la Muungano 2026. Hii inaongeza uzito wa michezo ya leo, huku kila timu ikihitaji ushindi ili kuendelea kubaki kwenye kinyang’anyiro cha ubingwa.
Mapendekezo ya Mhariri:








Leave a Reply