Ratiba ya Simba Sc Ligi Kuu Ya NBC 2024/2025 | Ratiba ya Michezo ya Simba Ligi Kuu Tanzania Bara
Msimu mpya wa Ligi Kuu ya NBC 2024/2025 unakaribia kuanza, na mashabiki wa soka kote nchini Tanzania wanasubiri kwa hamu kuona jinsi wekundu wa msimbazi Simba Sc watakavyo fanya. Kwa Simba SC, Msimu huu mpya unatazamiwa kua ndio msimu wa timu hii kurudisha ubabe wake na kubeba ubingwa kwa mara nyengine. Ratiba ya mechi imetoka, na sasa tunaweza kuona ni vipi safari yao itaanza.
Katika msimu huu wa 2024/2025, Simba SC itakuwa ikiutumia uwanja wa KMC Complex, Mwenge, kama uwanja wao wa nyumbani.
Ratiba ya Simba Sc Ligi Kuu Ya NBC 2024/2025
Ratiba ya mechi za Ligi Kuu imetoka, na mechi tano za kwanza za Simba SC ni kama ifuatavyo:
- Simba SC vs Tabora United (KMC Complex)
- Simba SC vs Fountain Gate (KMC Complex)
- Prisons vs Simba SC (Sokoine)
- Azam FC vs Simba SC (Benjamin Mkapa)
- Simba SC vs Namungo FC (KMC Complex)
Mechi hizi za kwanza zitakuwa kipimo muhimu kwa Simba SC. Watahitaji kuanza msimu kwa ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea taji lao. Mechi dhidi ya Azam FC na Prisons zitakuwa ngumu haswa, kwani hizi ni timu zenye ushindani mkubwa.
Hii Apa Ratiba ya Simba Sc Ligi Kuu Ya NBC 2024/2025
Tarehe | Nyumbani | Dhidi | Ugenini | Muda | Dimba |
18-Aug-24 | Simba SC | VS | Tabora United | 16:15 | KMC Complex |
25-Aug-24 | Simba SC | VS | Fountain Gate | 16:00 | KMC Complex |
– | Azam FC | VS | Simba SC | TBA | Benjamin Mkapa |
TBA | Simba SC | VS | Namungo FC | TBA | KMC Complex |
4-Oct-24 | Simba SC | VS | Coastal Union | 16:15 | KMC Complex |
19-Oct-24 | Simba SC | VS | Young Africans | 17:00 | KMC Complex |
– | Mashujaa FC | VS | Simba SC | TBA | Lake Tanganyika |
TBA | Simba SC | VS | JKT Tanzania | TBA | KMC Complex |
– | Simba SC | VS | KMC FC | TBA | TBA |
21-Nov-24 | Pamba Jiji | VS | Simba SC | 16:15 | CCM Kirumba |
Mapendekezo ya Mhairi:
Weka Komenti