Matokeo ya Yanga Vs Simba Leo Ngao Ya Jamii 08/08/2024

Matokeo ya Yanga Vs Simba Leo Ngao Ya Jamii 08/08/2024 | Matokeo ya Simba Vs Yanga Leo | Matokeo ya Mechi ya Yanga dhidi ya Simba Leo Ngao ya Jamii 2024

Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara mara tatu mfuluzizo Yanga Sc leo watachuana vikali na mabingwa watetezi wa michuano ya Ngao ya Jamii Simba SC katika mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya jamii msimu wa 2024. Mechi hii imepangwa kuchezeka leo Agosti 08 2024 katika dimba la Benjamin mkapa majira ya saa 01 usiku. Timu hizi mbili zimekutana mara tisa katika Ngao ya Jamii, huku Simba wakiibuka washindi mara tano na Yanga mara nne. Mwaka jana, Simba walinyakua taji hilo kwa mikwaju ya penalti baada ya sare tasa.

Yanga, chini ya kocha Miguel Gamondi, watauingia mchezo huu wakiwa na kiu ya kulipiza kisasi na kudhihirisha ubora wao dhidi ya Simba licha ya kufanya hivyo katika michezo ya ligi ya msimu uliopita. Kocha Gamondi ameweka wazi kuwa kipaumbele chake kikuu ni Ligi Kuu na michuano ya kimataifa, lakini ushindi dhidi ya watani wao wa jadi utakuwa ni mwanzo mzuri wa msimu.

Simba, wakiongozwa na kocha mpya Fadlu Davids, watakuwa na shinikizo la kutetea taji lao na kuendeleza utawala wao katika soka la Tanzania. Davids, ambaye anachukua mikoba ya Abdelhak Benchikha, anajua umuhimu wa mechi hii kwa mashabiki na uongozi wa Simba.

Wachezaji wapya wa Simba, akiwemo mshambuliaji hatari  Debora Fernandez, Jean Charles Ahoua na Mutale wanatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa katika kikosi hicho. Yanga nao wameimarisha kikosi chao kwa usajili wa wachezaji wenye uzoefu kama Prince Dube.

Matokeo ya Yanga Vs Simba Leo Ngao Ya Jamii 08/08/2024

Hapa chini tutakuletea live Matokeo ya Mechi ya Yanga dhidi ya Simba Leo Ngao ya Jamii 2024

Yanga Sc 1-0 FT Simba Sc
  • 45’— ⚽️ Maxi Nzingeli
  • Dak 38 Kadi ya kwanza ya Njano inakwenda kwa Khalid Aucho
  • Dak 15’ Pacome anafanyiwa faulo
  • Dak 03 Prince Dube anagongesha mwamba
  • Dak 02’ Kapombe anapoteza nafasi ya wazi.

Hili Apa Goli La Maxi

  • 🏆 #Ngao Ya Jamii🇹🇿
  • ⚽️ Young Africans SC🇹🇿🆚Simba SC🇹🇿
  • 📆 08.08.2024
  • 🏟 Uwanja wa Benjamin Mkapa
  • 🕖 Saa Moja Usiku🇹🇿

Angalia Vikosi Hapa Chini

  1. Kikosi cha Simba Vs Yanga Ngao Ya Jamii 08/08 2024
  2. Kikosi cha Yanga Vs Simba Ngao Ya Jamii 08/08/2024

Mchezo huu wa leo utakuwa ni wa nne mfululizo wa Ngao ya Jamii kati ya Simba na Yanga tangu mwaka 2021. Katika kipindi hiki, Yanga imeshinda michezo miwili na Simba mmoja. Hivyo, ushindani unatarajiwa kuwa mkubwa sana, hasa kwa kuwa Simba inataka kuleta ushindi ili kulipa kisasi na kuweka rekodi sawa kwenye mashindano hayo.

Simba inatarajia kubeba taji lao la 11 la Ngao ya Jamii na kuwapita zaidi watani wao Yanga. Wakati huo huo, Yanga inataka kuendeleza ubabe mbele ya Simba baada ya kushinda michezo miwili ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2023-2024 kwa jumla ya mabao 7-2. Katika mechi hizo, Yanga ilishinda 5-1 dhidi ya Simba na baadaye 2-1.

Matokeo ya Yanga Vs Simba Leo Ngao Ya Jamii 08/08/2024

Kauli za Makocha

Makocha wa pande zote mbili wametoa kauli zao kuelekea mchezo huu. Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi, amesisitiza kuwa kipaumbele chake ni Ligi Kuu na michuano ya kimataifa, huku akitumia Ngao ya Jamii kama sehemu ya maandalizi ya msimu. Kwa upande mwingine, Kocha Fadlu Davids wa Simba ameonyesha dhamira ya kuanza msimu kwa ushindi na kutetea taji la Ngao ya Jamii.

Historia ya Michuano ya Ngao ya Jamii

Ngao ya Jamii imekuwa ikiandaliwa tangu mwaka 2001, ingawa haikuchezwa katika miaka ya 2004, 2006, 2007, na 2008. Mpaka sasa, zimechezwa jumla ya fainali 19 za Ngao ya Jamii. Mara ya kwanza timu hizi zilipokutana kwenye michuano hii, Yanga ilishinda kwa mabao 2-1, yaliyofungwa na Edibily Lunyamila na Ally Yusuph ‘Tigana’, huku bao la Simba likifungwa na Steven Mapunda ‘Garincha’. Mara ya mwisho walipokutana, Simba iliibuka mshindi kwa mikwaju ya penalti 3-1 baada ya dakika tisini kumalizika bila mabao.

Matokeo Ya Michezo Yote Ya Fainali ya Ngao Ya Jamii

  • 2001 Yanga 2-1 Simba
  • 2002 Simba 4-1 Yanga
  • 2003 Simba 1-0 Mtibwa
  • 2004 HAIKUFANYIKA
  • 2005 Simba 2-0 Yanga
  • 2006-2008 HAIKUFANYIKA
  • 2009 Mtibwa 1-0 Yanga
  • 2010 Yanga 0-0 Simba (penalti 3-1)
  • 2011 Simba 2-0 Yanga
  • 2012 Simba 3-2 Azam
  • 2013 Yanga 1-0 Azam
  • 2014 Yanga 3-0 Azam
  • 2015 Yanga 0-0 Azam (penalti 8-7)
  • 2016 Azam 2-2 Yanga (penalti 4-1)
  • 2017 Simba 0-0 Yanga (penalti 5-4)
  • 2018 Simba 2-1 Mtibwa
  • 2019 Simba 4-2 Azam
  • 2020 Simba 2-0 Namungo
  • 2021 Yanga 1-0 Simba
  • 2022 Yanga 2-1 Simba
  • 2023 Simba 0-0 Yanga (penalti 3-1)

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Matokeo ya Ngao ya Jamii 2024
  2. Washindi wa Ngao ya Jamii Miaka Yote
  3. Vituo vya Kukata Tiketi Mechi ya Ngao ya Jamii Yanga vs Simba
  4. Nchi za Afrika Zilizopata Medali za Olympics 2024
  5. Rekodi za Simba na Yanga Kufungana
  6. Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025 (NBC Premier league)
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo