Ratiba ya yanga Klabu Bingwa CAF 2024/2025

Ratiba ya yanga Klabu Bingwa CAF 2024/2025 | Ratiba ya Yanga Sc CAF Champions league 2024/25

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania, Yanga SC, wapo tena kwenye mstari wa mbele kuiwakilisha nchi katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika (CAF Champions League) kwa msimu wa 2024/2025.

Katika misimu miwili iliyopita, Yanga imeonyesha uwezo wa hali ya juu kwenye ngazi ya kimataifa, ikiwemo kufika fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF msimu wa 2022/2023 na hatua ya robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika msimu uliopita, ambapo walitolewa kwa mikwaju ya penalti na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Msimu huu, matarajio ni makubwa zaidi kwa mashabiki wa Yanga SC baada ya usajili wa wachezaji wapya wenye vipaji vya hali ya juu, ambao wamejiunga na kikosi chenye uzoefu wa michuano hii mikubwa. Yanga imejipanga vilivyo kuhakikisha inaendelea kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika mashindano haya.

Ratiba ya yanga Klabu Bingwa CAF 2024/2025

Yanga imeanza safari yao ya klabu bingwa Afrika katika hatua ya awali ambapo watachezaja jumla ya mechi nne dhidi ya wapinzani wawili. Mechi mbili za kwanza zitachezwa dhidi ya Vital’o ya Burundi na mbili nyengine zitachezwa dhidi ya CBE SA ambao wamefuzu roundi ya pili ya hatua ya awali ya CAF Champions league baada ya kuitoa SC Villa ya Uganda.

Ratiba ya Yanga Raundi ya Kwanza Hatua za Awali Klabu Bingwa

Katika mzunguko wa kwanza wa hatua ya awali ya michuano ya klabu bingwa Afrika, Yanga ilikutana na Vital’O kutoka Burundi, ambapo walicheza mechi mbili kama ifuatavyo:

TareheMechiUwanja
17 Agosti 2024Vital’O vs YangaAzam Complex, Dar es Salaam
24 Agosti 2024Yanga vs Vital’OBenjamin Mkapa Stadium, Dar es Salaam

Ratiba ya yanga Klabu Bingwa CAF 2024/2025

Baada ya kuibuka washindi kwa jumla ya mabao 10-0 dhidi ya Vital’O, Yanga SC imefuzu hatua ya pili ya michuano ya Klabu Bingwa CAF.

Ratiba ya Yanga Raundi ya Pili Hatua za Awali Klabu Bingwa

Mabingwa wa Tanzania sasa watakutana na CBE SA ya Ethiopia katika hatua ya pili. Mechi hizi zinatarajiwa kuanza kama ifuatavyo:

  • Mechi ya Kwanza: Yanga vs CBE SA – Tarehe 13 Septemba 2024, Zanzibar katika Uwanja wa New Amaan Complex
  • Mechi ya Pili: CBE SA vs Yanga – Tarehe 27 Septemba 2024, Addis Ababa Stadium, Ethiopia.

Mashabiki wa Yanga SC wana matumaini makubwa msimu huu, wakitegemea kuona timu yao ikisonga mbele zaidi katika michuano hii ya kifahari barani Afrika. Kikosi kimeongezewa nguvu na wachezaji wapya, na Kocha amejizatiti kuhakikisha kuwa timu inafikia malengo yake ya kutwaa ubingwa wa Afrika kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu.

Ratiba ya Yanga Hatuia ya Makundi Klabu Bingwa Afrika

  • 26/11/2024: Yanga vs Al Hilal.
  • 06/12/2024: MC Alger vs Yanga
  • 13/12/2024: TP Mazembe vs Yanga
  • 03/01/2025: Yanga vs TP Mazembe
  • 10/01/2025: Al Hilal vs Yanga
  • 17/01/2025: Yanga vs MC Alger.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ratiba ya Mechi za Yanga Ligi Kuu NBC 2024/2025
  2. Ratiba ya Mechi Zijazo za Yanga 2024/2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo