Seif Karihe Acharazwa Faini na Kufungiwa Michezo Mitatu kwa Kurusha Chupa

Seif Karihe Acharazwa Faini na Kufungiwa Michezo Mitatu kwa Kurusha Chupa

Mchezaji wa klabu ya Mashujaa FC, Seif Abdallah maarufu kwa jina la Karihe, amejikuta matatani baada ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kumpiga marufuku ya kutocheza michezo mitatu mfululizo, sambamba na faini ya shilingi 500,000. Haya ni matokeo ya kitendo chake cha utovu wa nidhamu ambapo alirushia mashabiki chupa za maji na kuingia mara kadhaa uwanjani kutoka benchi la timu hiyo, akimlalamikia mwamuzi wa mchezo.

Tukio hilo linalozua mjadala lilitokea Mei 2, 2025, katika uwanja wa KMC Complex wakati wa pambano la Ligi Kuu ya NBC kati ya Simba SC na Mashujaa FC, ambalo Simba walishinda kwa mabao 2-1.

Seif Karihe, ambaye ni mmoja wa wachezaji tegemeo wa Mashujaa, alionekana mara kadhaa akikimbilia uwanjani kutoka kwenye benchi akielekea kwa mwamuzi, kitendo kilichoonekana kuwa ni kinyume na maadili ya mchezo.

Kamati ya TPLB, katika kikao chake kilichofanyika Juni 2, 2025, ilichambua kwa kina matukio yote yaliyotokea katika mechi hiyo namba 190 ya Ligi Kuu, na kuafiki kuwa Seif Abdallah alivunja Kanuni ya 41:5(5.3) ya Ligi Kuu Tanzania Bara inayohusu Udhibiti kwa Wachezaji. Kutokana na hilo, Kamati hiyo ilimchukulia hatua kali kama njia ya kuweka mfano kwa wachezaji wengine na kulinda heshima ya mchezo.

Mtunza Vifaa wa Mashujaa FC Naye Aingia Kwenye Kichapo cha Adhabu

Mbali na adhabu dhidi ya Seif Karihe, Kamati hiyo pia imemchukulia hatua Mtunza Vifaa wa klabu ya Mashujaa, Juma Nyenje, kwa kosa la kurusha chupa za maji kuelekea kwa mashabiki katika uwanja huo huo na siku hiyo hiyo. Nyenje amefungiwa kwa kipindi cha miezi sita (6) na pia kutozwa faini ya shilingi 500,000.

Adhabu dhidi ya Juma Nyenje imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 46:3 ya Ligi Kuu Tanzania Bara inayohusu Udhibiti kwa Viongozi. Hatua hii inaonesha dhahiri kuwa nidhamu ni jambo lisilo na mjadala katika uendeshaji wa ligi ya kitaifa, na viongozi wa timu wanapaswa kuwa mfano bora kwa wachezaji na mashabiki.

Seif Karihe Acharazwa Faini na Kufungiwa Michezo Mitatu kwa Kurusha Chupa

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Matokeo ya Germany Vs Portugal Leo 04/06/2025
  2. Wachezaji wa Soka U-21 Waliofanya Vizuri Msimu wa 2024/2025
  3. Mabekio Waliochangia Magoli Mengi Ligi Kuu ya NBC 2024/2025
  4. Siku ya Kuripoti Chuo cha Polisi Moshi 2025 kwa Vijana Waliochaguliwa
  5. Michezo ya Yanga Sc Iliobaki Msimu wa 2024/2025
  6. Wachezaji wa Yanga Walioitwa Kwenye Kikosi cha Timu ya Taifa June 2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo