Sifa za Kujiunga na Chuo Kikuu Cha UDSM 2025/2026

Sifa za Kujiunga na Chuo Kikuu Cha UDSM 2025/2026

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (University of Dar es Salaam – UDSM) ni taasisi ya elimu ya juu kongwe na ya kwanza kabisa kuanzishwa nchini Tanzania, kikianza rasmi mwaka 1970 baada ya kujitenga na Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki. Kwa kipindi cha zaidi ya nusu karne, UDSM kimeendelea kuwa nguzo kuu ya utafiti, ufundishaji na utoaji wa maarifa ya kisasa kwa maelfu ya wanafunzi wa ndani na nje ya nchi.

Chuo hiki kinatambulika si tu kwa umahiri wake katika taaluma mbalimbali bali pia kwa mchango wake mkubwa katika kuzalisha wataalamu waliobobea katika sekta za umma na binafsi.

UDSM kinapewa heshima kubwa kutokana na ubora wa mitaala yake, uwezo wa wahadhiri wake, mazingira bora ya kujifunzia, pamoja na miundombinu ya kisasa inayowawezesha wanafunzi kujifunza kwa ufanisi. Kutokana na sifa hizo, UDSM kimeendelea kuvutia maombi mengi kila mwaka kutoka kwa wanafunzi wanaotamani kupata elimu bora ya juu.

Kwa mwaka wa masomo 2025/2026, chuo hiki kinakaribisha maombi kutoka kwa vijana wa Kitanzania na wale wa kimataifa wanaotaka kujiunga na shahada ya kwanza katika programu mbalimbali za kitaaluma zinazotolewa katika vyuo na shule zake 15 zilizopo ndani ya kampasi kuu ya Mlimani na kampasi nyingine zilizoko Iringa, Mbeya, Dodoma, Nzega, na Zanzibar.

Makala hii itaeleza kwa kina sifa zinazohitajika ili kujiunga na Chuo Kikuu cha UDSM kwa ngazi ya shahada ya kwanza kwa mwaka wa masomo 2025/2026, ikijumuisha:

  1. Vigezo vya jumla vya udahili,
  2. Sifa maalum kwa kila kozi na chuo/shule,
  3. Maelekezo kwa waombaji wa moja kwa moja (Form VI),
  4. Vigezo vya waombaji wa diploma au vyeti vya kitaalamu.

Kupitia mwongozo huu, waombaji wataweza kujitathmini mapema kabla ya kutuma maombi yao rasmi. Hii ni hatua muhimu katika kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaingia kwenye programu ambazo wamekidhi vigezo vinavyohitajika, kwa kuzingatia matokeo yao, taaluma waliyosomea awali, pamoja na matakwa ya kitaaluma ya kila kozi.

Sifa za Kujiunga na Chuo Kikuu Cha UDSM 2025/2026

Sifa za Jumla za Kujiunga na Chuo Kikuu Cha UDSM 2025/2026

Kama wewe ni miongoni mwa maelfu ya wahitimu wa Kidato cha Sita au Diploma wenye ndoto ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), basi kuzijua sifa zinazohitajika ni hatua ya kwanza na muhimu katika safari yako ya kutuma maombi. Ili maombi yako ya kujiunga na chuo hiki maarufu yakubalike, unapaswa kukidhi vigezo vya jumla vilivyowekwa na chuo kwa ajili ya waombaji wa shahada ya kwanza.

Kumbuka: Chuo cha UDSM kina ushindani mkubwa katika udahili wa wanafunzi. Hivyo, kukidhi vigezo vilivyowekwa hakuhakikishi moja kwa moja kupokelewa au kuchaguliwa kujiunga na chuo hiki. Matokeo mazuri ya mtihani ndiyo yanayopewa kipaumbele kikubwa katika mchakato wa uteuzi wa waombaji.

A. Waombaji wa Moja kwa Moja (Direct Entry – Kidato cha Sita)

Waombaji waliomaliza elimu ya sekondari ngazi ya Kidato cha Sita (ACSEE) wanapaswa kuwa na:

Cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) chenye ufaulu wa masomo matano yaliyoidhinishwa, ambapo angalau matatu kati ya hayo lazima yawe na alama ya credit (daraja la ‘C’ au zaidi).

Cheti cha Kidato cha Sita (ACSEE) chenye alama mbili za principal kutoka katika masomo yanayohusiana na kozi anayoiomba. Jumla ya pointi za principal hizo lazima ziwe 4.0 au zaidi, kulingana na mfumo wa upangaji wa alama ufuatao:

  • Kwa wahitimu wa mwaka 2016 na kuendelea:
    A = 5, B = 4, C = 3, D = 2, E = 1
  • Kwa wahitimu wa 2014 na 2015:
    A = 5, B+ = 4, B = 3, C = 2, D = 1, E = 0.5

Angalizo: Daraja la chini kabisa linalokubalika kama principal ni “E” kwa wahitimu wa 2016 na kuendelea, na “D” kwa wahitimu wa 2014/2015.

B. Sifa za Kujiunga na Chuo Kikuu Cha UDSM 2025/2026 Kwa Waombaji wa Diploma (Equivalent Entry)

Kwa waombaji waliomaliza Diploma katika vyuo vinavyotambuliwa na NACTVET na Seneti ya UDSM:

  • Sharti la GPA: Lazima wawe na alama ya wastani (GPA) isiyopungua 3.5, au
  • Wastani wa Daraja la ‘B’ au ‘B+’, au
  • Daraja la ‘Distinction’ kwa vyeti visivyoainisha GPA, au
  • Daraja la Upper Second Class kwa diploma zisizo katika mfumo wa NTA.

Muhimu: Diploma lazima iwe katika fani husika au inayohusiana na kozi unayoomba, na taasisi iliyotoa cheti hicho iwe imesajiliwa rasmi na kutambuliwa na mamlaka husika.

C. Waombaji wa Kimataifa

Kwa waombaji kutoka nje ya Tanzania, hasa kutoka nchi zinazotumia mfumo wa elimu wa 8-4-4, wanapaswa kuwa wamekamilisha angalau mwaka mmoja wa masomo ya shahada katika chuo kikuu kilichopo nchini mwao kabla ya kuwasilisha maombi ya kujiunga na UDSM.

Sifa Maalum kwa Kila Kozi Kulingana na Shule au Chuo

Mbali na sifa za jumla zilizo orodheshwa hapo juu, kuna sifa maalumu ambazo zinatofautiana kulingana na kozi inayoombwa. Hii ni kwa sababu kila programu ya shahada ya kwanza ina mahitaji yake ya kiakademia yanayolenga kuhakikisha kuwa mwanafunzi ana msingi sahihi wa taaluma husika kabla ya kuanza masomo ya ngazi ya chuo kikuu.

Kwa urahisi wa waombaji wote, hapa chini tumekuletea muhtasari wa sifa maalumu kwa kozi zote zinazotolewa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa mwaka wa masomo 2025/2026, kwa kuzingatia kile kilichowasilishwa rasmi katika PDF ya Prospectus ya Shahada ya Kwanza.

A. College of Agricultural Sciences and Food Technology (CoAF)

BSc in Beekeeping Science and Technology

  • Direct Entry: Principal mbili, moja ya somo la Biology na moja kati ya Chemistry, Nutrition, Agriculture, Physics au Geography.
  • Equivalent: Diploma ya Sayansi ya Biolojia kama Ufugaji Nyuki, Kilimo, Uvuvi, Misitu n.k. GPA si chini ya 3.5.

BSc in Agricultural Engineering and Mechanization

  • Direct Entry: Principal mbili katika masomo ya Mathematics na Physics.
  • Equivalent: Diploma ya Uhandisi kama Civil, Mechanical, Electrical au Water Resources Engineering, GPA ≥ 3.5.

BSc in Food Science and Technology

  • Direct Entry: Biology na mojawapo ya Chemistry, Nutrition, Agriculture, Physics au Geography. Pia lazima awe na credit ya Mathematics O-Level na subsidiary A-Level.
  • Equivalent: Diploma ya sayansi ya viumbe (kama Kilimo, Misitu n.k.) na GPA ≥ 3.5, credit ya Mathematics O-Level ni lazima.

BSc in Agricultural and Natural Resources Economics and Business

  • Direct Entry: Principal mbili kati ya Economics, Commerce, Agriculture, Geography au Mathematics.
  • Equivalent: Diploma ya fani husika na GPA ≥ 3.5.

B. College of Engineering and Technology (CoET)

Kozi Zote za Uhandisi (isipokuwa BSc in Textile Design & Architecture)

  • Direct Entry: D grade au zaidi katika Mathematics na Physics, na subsidiary pass au credit ya Chemistry.
  • Equivalent: Diploma ya kiufundi yenye GPA ≥ 3.5 na daraja la C au zaidi katika Mathematics.

BSc in Textile Design and Technology

  • Direct Entry: D katika masomo yoyote ya Sayansi au Sanaa (ikiwemo Fine Arts), na credit ya Chemistry na Mathematics.
  • Equivalent: Diploma yoyote yenye GPA ≥ 3.5.

Bachelor of Architecture

  • Direct Entry: Principal mbili kati ya Physics, Chemistry, Biology, Mathematics, Geography au Fine Arts. Credit ya Mathematics ni lazima.
  • Equivalent: Diploma husika yenye GPA ≥ 3.5.

C. College of Humanities (CoHU)

BA in History

  • Direct Entry: Principal moja lazima iwe History (D au zaidi), nyingine kutoka masomo kama English, Kiswahili, Economics, n.k.
  • Equivalent: Diploma ya Archival Studies, Records Management, Library Science n.k., GPA ≥ 3.5.

BA in History and Political Science

  • Direct Entry: History (C au zaidi) na moja nyingine kati ya English, Kiswahili, Economics, Geography, n.k.
  • Equivalent: Diploma ya International Relations, Legal Studies, n.k., GPA ≥ 3.5.

D. College of Information and Communication Technologies (CoICT)

BSc in Computer Science / IT / Telecommunication / Electronics

  • Direct Entry: Principal mbili – Mathematics na Physics.
  • Equivalent: Diploma inayohusiana, GPA ≥ 3.5 au B+.

BSc in Business Information Technology

  • Direct Entry: Principal mbili kutoka Mathematics, Physics, Chemistry, Biology au Economics. Ikiwa huna Advanced Mathematics, lazima uwe na C katika Mathematics O-Level.
  • Equivalent: Diploma ya IT, Computer Engineering, Statistics, Economics n.k., GPA ≥ 3.5.

Soma Sifa za Kujiunga na Kozi Nyengine Kwenye PDF Hapa Chini

Sifa za Kujiunga Chuo cha UDSM

Jinsi ya Kutuma Maombi Chuo Kikuu cha UDSM 2025/2026

Kwa mwaka wa masomo 2025/2026, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinapokea maombi ya kujiunga na shahada ya kwanza kupitia mfumo wa kielektroniki unaojulikana kama UDSM-OLAS (Online Admission System). Mfumo huu unapatikana kupitia tovuti rasmi ya chuo:

🔗 https://admission.udsm.ac.tz
🔗 https://www.udsm.ac.tz

Waombaji wote—wa moja kwa moja (Direct Entry) na wenye sifa mbadala (Diploma au vyeti)—lazima watume maombi kupitia UDSM-OLAS pekee.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Dirisha la Maombi ya Vyuo Vikuu 2025/2026 Lafunguliwa Rasmi – Tuma Maombi Kabla ya 10 Agosti
  2. Sifa za Kujiunga na Chuo Cha Uhasibu TIA 2025/2026
  3. Sifa za Kujiunga na Vyuo Mbalimbali Tanzania 2025/2026
  4. Vigezo vya Kupata Mkopo Ngazi ya Diploma 2025/2026
  5. Matokeo ya Kidato cha Sita 2025 NECTA ACSEE
  6. Mwisho wa Kutuma Maombi ya Mkopo 2025/2026
  7. Kozi za Diploma Zenye Mkopo 2025/2026
  8. HESLB Yatangaza Kufunguliwa kwa Dirisha la Maombi ya Mikopo 2025/2026
  9. Matokeo ya Kidato cha Sita 2025 (NECTA Form Six Results)
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo