Matokeo ya Pamba Jiji Vs Tanzania Prisons Leo 16/08/2024 | Matokeo Mechi ya Pamba Dhidi ya Tanzania Prisons Leo
Pazia la Ligi Kuu ya NBC Tanzania msimu wa 2024/2025 litafunguliwa rasmi tarehe 16 Agosti 2024 kwa pambano kali kati ya Pamba Jiji na Tanzania Prisons. Mchezo huu wa ufunguzi utapigwa katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, majira ya saa 10 jioni. Mashabiki wa soka nchini wanatarajia mechi hii kuwa na ushindani mkubwa kutokana na maandalizi na usajili wa nguvu uliofanywa na timu zote mbili.
Pamba Jiji: Historia na Matarajio
Pamba Jiji ni timu yenye historia ndefu katika soka la Tanzania, lakini msimu uliopita wa 2023/2024 walikuwa wakipambana katika Ligi Daraja la Kwanza (Championship). Walimaliza msimu huo kwa mafanikio makubwa na kufanikiwa kupanda daraja, jambo linalowafanya kuwa na morali kubwa kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu. Mashabiki wa Pamba Jiji wanatarajia kuanza ligi kwa ushindi, wakitegemea kuwa na kikosi imara kitakachoweza kupambana na miamba ya Ligi Kuu.
Tanzania Prisons: Changamoto na Malengo
Tanzania Prisons, ambao wamekuwa washiriki wa kudumu wa Ligi Kuu, wapo tayari kwa msimu mpya na wamejipanga kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya Pamba Jiji. Kwa kuwa na uzoefu wa kucheza Ligi Kuu kwa miaka kadhaa, Tanzania Prisons wanaingia katika mchezo huu wakiwa na nia thabiti ya kuhakikisha wanapata pointi zote tatu na kuanza msimu mpya kwa mafanikio.
Matokeo ya Pamba Jiji Vs Tanzania Prisons Leo 16/08/2024
Pamba Jiji Fc | 0-0 FT | Tanzania Prisons |
- 🏆 #Ligi Kuu Ya NBC 2024/2025
- ⚽️ Pamba Jiji🆚Tanzania Prisons Fc
- 📆 16.08.2024
- 🏟 Uwanja wa CCM Kirumba
- 🕖 4:00PM
Angalia Hapa Vikosi Mechi ya Pamba Jiji Vs Tanzania Prisons 16/08/2024
Kocha wa Pamba Jiji, Goran Kopunovic amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kesho katika dimba la CCM Kirumba, kwa ni siku hiyo ni ya kihistoria. Pamba Jiji FC itavaana na Tanzania Prisons kwenye mchezo wa ufunguzi wa NBC Premier League msimu wa 2024/25. Nahodha wa timu hiyo Christopher Oruchum amewaomba mashabiki kwenda kuishuhudia mechi hiyo ili kuwapa hamasa.
Viingilio na Namna ya Kukata Tiketi
Mashabiki watakaohudhuria mchezo huu wana fursa ya kuchagua viingilio vinavyowafaa. Viingilio ni kama ifuatavyo:
- VIP: TZS 10,000
- Jukwaani: TZS 5,000
- Mzunguko: TZS 2,000
Kwa wale ambao hawajakamilisha ununuzi wa tiketi mapema, tiketi zinapatikana katika maeneo yafuatayo:
- Ofisi kuu za Halmashauri ya Jiji Mwanza
- Ofisi za TTCL-Mwanza
- Uwanja wa CCM Kirumba
- Gari ya Matango
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti