Silver Strikers vs Yanga Sc Leo 18/10/2025 Saa Ngapi?
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania, Yanga SC, leo watashuka dimbani kwa mara nyingine kupeperusha bendera ya taifa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika (CAF Champions League). Wanajangwani hao watakuwa ugenini nchini Malawi, wakipambana na Silver Strikers katika mchezo muhimu wa raundi ya pili ya hatua za awali ya michuano hiyo. Mchezo huu wa kukata na shoka unatarajiwa kuchezwa leo tarehe 18 Oktoba 2025 majira ya saa 10:00 jioni (16:00) kwa saa za Afrika Mashariki.
Silver Strikers vs Yanga Sc Leo 18/10/2025 Saa Ngapi?
Mashabiki wengi wa soka barani Afrika, hasa kutoka Tanzania na Malawi, wanajiuliza kwa hamu kubwa: Silver Strikers vs Yanga Sc leo ni saa ngapi? Kwa mujibu wa taarifa rasmi, mchezo huu utapigwa saa 10:00 jioni (16:00) kwa saa za Afrika Mashariki.
Huu ni mchezo wa raundi ya pili ya awali (2nd Preliminary Round), ambapo Yanga SC itakuwa ugenini ikisaka matokeo mazuri kabla ya mchezo wa marudiano utakaopigwa jijini Dar es Salaam.
Ratiba na Taarifa Muhimu za Mchezo
- Mchezo: Silver Strikers vs Yanga SC
- Tarehe: Jumamosi, 18 Oktoba 2025
- Saa: 10:00 Jioni (16:00 EAT)
- Mahali: Malawi
- Mashindano: Ligi ya Mabingwa Afrika – Raundi ya Pili ya Awali
Maandalizi ya Yanga SC Kabla ya Safari
Kikosi cha Yanga SC kiliondoka mapema asubuhi ya tarehe 16 Oktoba 2025, kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam, kuelekea Malawi. Safari hii ni sehemu ya maandalizi makini ya klabu hiyo inayolenga kuhakikisha inapata matokeo chanya katika uwanja wa ugenini kabla ya kurudi nyumbani kwa mchezo wa marudiano.
Ofisa Habari wa klabu hiyo, Ali Kamwe, amethibitisha maandalizi hayo na kueleza kuwa timu iko tayari kwa changamoto hiyo muhimu ya kimataifa. Hata hivyo, Kamwe ameonya kwamba mchezo huo hautakuwa rahisi, kutokana na ubora na motisha ya wapinzani wao kutoka Malawi.
Kauli ya Ofisa Habari wa Yanga – Ali Kamwe
Kwa mujibu wa Ali Kamwe, licha ya Yanga kuwa na kocha msaidizi Patrick Mabedi, ambaye anatoka Malawi, bado mechi hiyo haitakuwa rahisi.
“Tunafahamu kuwa Silver Strikers wataingia kwa nguvu kubwa, hasa kwa kuwa wanataka kuonyesha uwezo wao mbele ya kocha wetu msaidizi ambaye ni raia wa Malawi na amewahi kuwa kocha wa timu ya taifa yao,” alisema Kamwe.
Hata hivyo, aliongeza kuwa Yanga SC ina kikosi imara, chenye uwezo wa kupambana katika mazingira yoyote, na anaamini wataleta matokeo mazuri kutoka ugenini.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Timu Zilizofuzu Kombe la Dunia 2026
- Msimamo wa Ligi Kuu Zanzibar PBZ 2025/2026
- Majina Ya Usaili Kusimamia Uchaguzi 2025 Jimbo La Temeke, Mbagala na Chamazi
- Pacome Anukia Kombe la Dunia Baada ya Ushindi 7-0 Dhidi ya Shelisheli
- Zimbabwe Yainyima Nafasi Afrika Kusini Kufuzu Kombe la Dunia
- Kaizer Chiefs Ya Thibitisha Kuachana na Kocha Nasreddine Nabi
- Msimamo wa Ligi kuu NBC Tanzania 2025/2026
Leave a Reply