Simba Sc vs KMC leo 11 May 2025 Saa Ngapi?

Simba Sc vs KMC leo 11 May 2025 Saa Ngapi

Simba Sc vs KMC leo 11 May 2025 Saa Ngapi?

Kikosi cha Mnyama Simba kitashuka dimbani Jumapili ya Mei 11, 2025 katika mchezo wa kiporo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya KMC FC. Mchezo huu utapigwa katika Uwanja wa KMC Complex, ukiwa ni wa mwisho kwa KMC kucheza nyumbani msimu huu. Hii ni mechi yenye matarajio makubwa kutokana na umuhimu wake kwa pande zote mbili—KMC ikisaka pointi muhimu za kujinusuru na kushuka daraja, na Simba ikiwania kuiweka hai ndoto yao ya ubingwa wa ligi kuu msimu huu wa 2024/2025.

Muda wa Mchezo: Saa Ngapi?

Kwa mujibu wa taarifa rasmi zilizotolewa, mchezo huu utaanza saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki. Mashabiki wanashauriwa kufika mapema viwanjani ili kushuhudia pambano hili la vuta nikuvute ambalo linaweza kuamua hatma ya msimu kwa baadhi ya timu hizi.

Simba Sc vs KMC leo 11 May 2025 Saa Ngapi?

Kaimu Kocha Mkuu wa KMC, Adam Mbwana, amesisitiza kuwa timu yake imejipanga kikamilifu kuikabili Simba SC. Akizungumza na wanahabari kabla ya mchezo, Mbwana alieleza kuwa wamekuwa na muda mzuri wa maandalizi na wamefanya tathmini ya kutosha ya mechi zilizopita za Simba, hali inayowapa ujasiri wa kutumia mapungufu ya wapinzani wao kupata ushindi.

“Tuna michezo minne kabla ya kumaliza ligi, na huu wa Simba ndio pekee uliobaki nyumbani. Ni lazima tuutumie vizuri kutafuta pointi tatu ambazo ni muhimu sana kwetu,” alisema Mbwana.

Kocha huyo ameahidi kutumia mbinu zote stahiki kuzima ubabe wa Simba, huku akitambua ukubwa wa timu hiyo lakini akiamini kwamba hakuna timu isiyo na mapungufu.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Napoli Yajipanga Kumsajili Jack Grealish Kutoka Man City
  2. KENGOLD Yapanga Kuipeleka Simba Ruvuma Juni 18
  3. Simba SC Yakata Tiketi Ligi ya Mabingwa Afrika 2025-2026 Baada ya Kufikisha Pointi 66
  4. Yanga Yashikilia Msimamo wa Kutocheza Dabi Licha Ya Majibu ya CAS
  5. Simba Yaitandika JKT na Kujiweka Kwenye Njia ya Ligi ya Mabingwa
  6. Matokeo JKT Tanzania vs Simba Leo 05/05/2025

 

Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo