Singida Black Stars Yatinga Raundi Ya Pili Kombe la Shirikisho Afrika

Singida Black Stars Yatinga Raundi Ya Pili Kombe la Shirikisho Afrika

Singida Black Stars imeandika historia kwa kufuzu raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) baada ya ushindi wa jumla wa mabao 3–1 dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda. Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Kigali, Singida Black Stars walishinda kwa bao 1–0 kabla ya kuhitimisha kazi nyumbani kwa ushindi wa 2–1 katika dimba la Azam Complex, Chamazi.

Ushindi huu umeonyesha uthabiti na maandalizi ya kikosi hicho kipya katika soka la kimataifa, na sasa kitakabiliana na mshindi kati ya Al Akhdar ya Libya na Flambeau du Centre ya Burundi. Warundi wanaonekana kuwa na nafasi kubwa kufuatia ushindi wa 2–1 kwenye mkondo wa kwanza, huku marudiano yakitarajiwa kuchezwa tarehe 28 Septemba 2025.

Singida Black Stars Yatinga Raundi Ya Pili Kombe la Shirikisho Afrika

Katika mchezo wa marudiano dhidi ya Rayon Sports, mashabiki wa soka walishuhudia mpira wa kiwango cha juu. Idriss Diomande alifungua ukurasa wa mabao dakika ya 38, na kumaliza kipindi cha kwanza kikiwa na msisimko mkubwa.

Ingawa Gloire Tambwe aliwasawazishia Rayon Sports dakika ya 44, Antony Tra Bi Tra alihakikisha Singida Black Stars wanamaliza salama baada ya kufunga bao la pili dakika ya 56. Kwa matokeo hayo, wawakilishi hao wa Tanzania waliibuka na ushindi wa 2–1 siku hiyo, na kwa jumla ya mabao 3–1 wakatinga hatua inayofuata ya mashindano ya CAF.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Real Madrid Yapoteza 2-5 Dhidi ya Atletico Madrid, Kichapo cha Kwanza kwa Xabi Alonso LaLiga
  2. Haaland Sasa ni Miongoni mwa Wafungaji Bora 10 wa Muda Wote Man City
  3. Simba vs Gaborone Leo 28/09/2025 Saa Ngapi?
  4. Yanga Yatinga Raundi ya Pili CAF Champions League Baada ya Ushindi wa 2-0
  5. Matokeo ya Yanga vs Wiliete SC Leo 27/09/2025
  6. KMKM Yatinga Raundi ya Pili ya CAF Baada ya Kuichapa AS Port ya Djibouti
  7. Sergio Busquets Atangaza Kustaafu Soka Mwishoni Mwa Msimu Huu
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo