Tarehe ya Kuripoti Kambini JKT Mujibu wa Sheria 2024: Huu Ndio Mwongozo Kamili kwa Wahitimu wa Kidato cha Sita
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limetoa wito kwa vijana wote waliohitimu kidato cha sita mwaka 2024 kujiunga na mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria. Mafunzo haya yatakayo fanyika kwa muda wa miezi mitatu, ni muhimu katika kujenga uzalendo, umoja wa kitaifa, na kuwapa vijana stadi za kazi na maisha zitakazowawezesha kuchangia katika maendeleo ya taifa letu.
Tarehe ya Kuripoti Kambini JKT Mujibu wa Sheria 2024
Vijana wote waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti kwenye makambi yao kuanzia tarehe 1 Juni hadi 7 Juni 2024. Hii ni fursa ya kipekee kwa vijana kujifunza na kukuza nidhamu, kujitolea, na uongozi.
Utaratibu wa Kujua Kambi Uliyopangiwa
JKT imeweka utaratibu rahisi wa kuwasaidia vijana kujua kambi walizopangiwa. Unaweza kutumia njia zifuatazo:
- Tovuti ya JKT: Tembelea tovuti rasmi ya JKT (www.jkt.go.tz) ambapo utapata orodha kamili ya majina ya vijana waliochaguliwa, makambi waliyopangiwa, na maeneo ya makambi hayo.
- Simu ya Mkononi (USSD): Piga *152*00# kisha uchague namba 8 (Elimu), ikifuatiwa na namba 5 (JKT). Ingiza namba ya shule yako uliyosoma, ikifuatiwa na majina yako matatu. Utapata taarifa ya kambi yako na eneo lake. Huduma hii inapatikana kwa mitandao yote ya simu.
Vifaa Muhimu vya Kuandaa Kabla ya kwenda Kambini JKT
Ili kuwa tayari kwa mafunzo, hakikisha una vifaa vifuatavyo:
- Bukta ya rangi ya bluu iliyokolea (dark blue): Yenye mpira kiunoni, mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini, na isiyo na zipu.
- Fulana ya rangi ya kijani (green vest)
- Raba za michezo: Rangi ya kijani au bluu.
- Shuka mbili za kulalia: Rangi ya bluu bahari.
- Soksi ndefu: Rangi nyeusi.
- Nguo za kuzuia baridi: Kwa wale waliopangiwa mikoa yenye baridi.
- Tracksuit: Rangi ya kijani au bluu.
- Nyaraka muhimu: Vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya uhitimu wa kidato cha nne, na nyaraka nyingine muhimu za masomo.
- Nauli: Hakikisha una nauli ya kutosha ya kwenda na kurudi kutoka kambini.
Mapendekezo Ya Mhariri:
Weka Komenti