Wachezaji wa Simba Walioitwa Kwenye Kikosi cha Timu ya Taifa June 2025
Wachezaji saba wa Simba SC wamefanikiwa kujumuishwa katika kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania, maarufu kama Taifa Stars, ambacho kitaingia kambini tarehe 2 Juni 2025 kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Bafana Bafana ya Afrika Kusini, pamoja na kushiriki mashindano ya COSAFA yatakayowakutanisha na timu za Eswatini na Madagascar.
Hatua hii ni uthibitisho mwingine wa kiwango bora ambacho wachezaji hawa wa Simba SC wamekuwa wakionyesha katika mitanange ya mashindano mbalimbali ya ndani na yale ya kimataifa kombe la shirikisho Afrika CAF. Uwepo wao kwenye kikosi cha Taifa Stars unaongeza nguvu na uzoefu muhimu kuelekea michezo hiyo muhimu ya mwezi Juni.
Hawa ndio wachezaji wa Simba SC walioitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars Juni 2025:
- Ally Salim – Kipa
- Shomari Kapombe – Beki
- Mohamed Hussein – Beki
- Abdulrazack Mohamed – Kiungo
- Yusuph Kagoma – Kiungo
- Yusuph Kagoma – Kiungo
- Kibu Denis – Mshambuliaji
Mapendekezo ya Mhariri:
- Hawa Apa Maofisa wa Mechi ya Nusu Fainali CRDB Bank Federation Cup 2024/2025
- Kikosi cha Taifa Stars kilichoitwa kambini Kuelekea COSAFA na Mechi ya Kirafiki
- Coastal Union Yapiga Hesabu Kali Kumchukua Anicet Kiazayidi
- Chelsea Yaipiga Bao Manchester United Usajili wa Liam Rory Delap
- Xabi Alonso Aahidi Kurejesha Ufalme wa Real Madrid
- Singida BS Yashindwa Kutamba Mbele ya Simba Ligi Kuu NBC
- Waliochaguliwa JKT Mujibu wa Sheria 2025 – Pakua PDF Hapa!
Leave a Reply