Yanga Kumenyana na Cosmopolitan Katika Mechi ya Kirafiki KMC Complex
Katika mwendelezo wa maandalizi yao kuelekea michezo ya ligi kuu uya NBC 2024/2025 na michuano ya klabu bingwa Africa CAF, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC, watashuka dimbani kesho Ijumaa kukabiliana na Cosmopolitan FC katika mchezo wa kirafiki utakaopigwa kwenye Uwanja wa Manispaa ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Mtanange huu unakuja ikiwa ni siku moja tu baada ya Yanga kuichapa Kiluvya FC mabao 3-0 katika mchezo mwingine wa kirafiki uliopigwa uwanjani hapo hapo. Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi, amepanga mechi hizi za kujipima nguvu ili kuwapa nafasi wachezaji ambao hawana majukumu ya timu za taifa kupata ‘game time’ na kujiweka fiti.
“Kwa sasa ni changamoto kwangu kukamilisha program za mazoezi ya kikosi changu kwa sababu anakosa nusu ya wachezaji wake ambao wako katika majukumu ya timu za Taifa,” alisema Gamondi. “Hivyo basi, mechi hizi za kirafiki zinasaidia sana.”
Kikosi cha Yanga kimesalia na takribani wachezaji 13 tu kutoka timu ya wakubwa, na wengine wakiwa ni vijana kutoka timu ya vijana. Hata hivyo, Gamondi anaamini kuwa hii ni fursa nzuri kwa vijana hawa kuonyesha uwezo wao na kujifunza kutoka kwa wachezaji wakubwa.
Mchezo dhidi ya Cosmopolitan unatarajiwa kuwa wa ushindani mkubwa, kwani timu hiyo inayoshiriki ligi ya Championship nayo itakuwa ikijiandaa kwa msimu mpya. Mashabiki wa soka wanatarajia kushuhudia mtanange wa kuvutia, huku Yanga wakitazamia kuendeleza wimbi lao la ushindi.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Nassor Saadun Hamoud Asaini Mkataba Mpya na Azam FC
- Clement Mzize: “Nina Hatari Zaidi Nikitokea Benchi”
- Messi na Ronaldo nje Ballon d’Or 2024
- Singida Black Stars Yafikia Makubaliano na Mwenda
- Picha za Jezi Mpya za Dodoma Jiji 2024/2025
- Wachezaji Sita wa Uingereza Watajwa Kwenye Orodha ya Ballon d’Or 2024
Weka Komenti