Yanga vs KMC Leo 09/11/2025 Sasa Ngapi?
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Young Africans (Yanga SC), leo wanashuka dimbani kuwakaribisha KMC FC katika mchezo unaotarajiwa kuwa wa ushindani mkubwa msimu wa 2025/2026. Pambano hilo ni miongoni mwa michezo inayosubiriwa kwa hamu, huku kila timu ikiwa na dhamira tofauti uwanjani Yanga ikisaka kurejea kileleni, na KMC FC ikipigania kutoka mkiani mwa msimamo wa ligi.
Mchezo huu wa Yanga vs KMC Leo 09/11/2025 utapigwa saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa KMC Complex, ambao unamilikiwa na KMC FC, licha ya Yanga kuonekana kama wenyeji wa mchezo huo leo.
Yanga inaingia kwenye mchezo huu ikiwa katika kiwango bora, ikikusanya pointi saba katika mechi tatu ilizocheza. Rekodi zao zinaonyesha uimara wa kiushindani, ikiwemo kutopoteza mchezo wowote kwa kuruhusu bao hadi sasa. Mabingwa hao wameshuhudia wavu wa wapinzani ukitikiswa mara tano, rekodi inayowafanya kuwa moja ya washambuliaji hatari kwenye ligi msimu huu.
Kwa upande mwingine, KMC FC imekuwa na mwanzo mgumu wa msimu. Timu hiyo imecheza mechi tano, lakini imepata pointi tatu pekee, hali iliyowafanya kushika nafasi za mkiani. Kocha wa KMC, Marcio Maximo, anaripotiwa kuwa kwenye shinikizo kubwa kutokana na mwelekeo wa matokeo ya timu hiyo, huku mijadala ya hatma yake ikizidi kuongezeka.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Ratiba ya Ligi Kuu Wanawake Tanzania (TWPL) 2025/2026
- Droo ya Makundi Kombe la Shirikisho Afrika CAF 2025/2026
- Yanga Yaangukia Kundi B na Al Ahly Droo ya Makundi Klabu Bingwa 2025/2026
- Msimamo Kundi la Yanga Klabu Bingwa 2025/2026
- Msimamo Kundi la Simba Klabu Bingwa 2025/2026
- Droo ya Makundi Klabu Bingwa Afrika 2025/2026









Leave a Reply