Ratiba ya Mechi za Robo Fainali CAF Champions League Wikiendi Hii

Ratiba ya Mechi za Robo Fainali CAF Champions League Wikiendi Hii

Ligi ya Mabingwa barani Afrika inaendelea kushika kasi huku mashabiki wa soka wakisubiri kwa hamu kubwa kuanza kwa hatua ya robo fainali ya CAF Champions League. Hatua hii muhimu ya mashindano inawaleta pamoja baadhi ya klabu bora kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika, huku kila timu ikilenga kusonga mbele kuelekea nusu fainali.

Kwa mujibu wa ratiba, mechi za robo fainali zinatarajiwa kuanza tarehe 13 Machi na kuendelea hadi Jumatatu tarehe 16 Machi, zikihusisha vilabu vinavyoshiriki katika pambano kali la kusaka ushindi katika michuano hiyo mikubwa zaidi ya ngazi ya klabu barani Afrika.

Ratiba ya Mechi za Robo Fainali CAF Champions League

Hatua ya robo fainali ya michuano ya CAF Champions League itaanza kwa mchezo mmoja siku ya Ijumaa kabla ya kuendelea katika siku zinazofuata. Hii hapa ni ratiba kamili ya mechi zinazotarajiwa kuchezwa wikiendi hii.

Ijumaa, 13 Machi

  • Mamelodi Sundowns vs Stade Malien
  • Saa 3:00 usiku

Jumamosi, 14 Machi

  • AS FAR vs Pyramids FC
  • Saa 7:00 usiku

Jumapili, 15 Machi

  • RS Berkane vs Al Hilal
  • Saa 7:00 usiku

Jumatatu, 16 Machi

  • ES Tunis vs Al Ahly
  • Saa 5:55 usiku

Ratiba ya Mechi za Robo Fainali CAF Champions League Wikiendi Hii

Hatua ya robo fainali mara nyingi huwa ni moja ya hatua zenye ushindani mkubwa katika CAF Champions League, kwani timu zote zilizosalia zinakuwa zimeonyesha kiwango cha juu tangu mwanzo wa mashindano. Mechi hizi zinatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na ubora wa vilabu vinavyoshiriki katika hatua hii.

Mashabiki wa soka barani Afrika wanatarajia kuona burudani ya hali ya juu wakati timu hizi zitakapokutana uwanjani katika pambano la kusaka nafasi ya kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ratiba ya 16 Bora Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup
  2. Mastaa Ligi Kuu Wavunja Rekodi Kombe la Shirikisho la CRDB Federation Cup
  3. Othmen Najjar Azungumzia Maandalizi ya Singida BS Kabla ya Kuivaa Yanga
  4. Azam vs Yanga Yaamishiwa Dimba la Chamazi
  5. Uwanja wa Mkapa Kufungwa Kupisha Maandalizi ya AFCON 2027
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo