Matokeo ya Mlandege VS Simba Leo 26/04/2026
Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi leo kinashuka dimbani kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya Kombe la Muungano dhidi ya Mlandege FC.
Mchezo huu unaamua ni timu gani kati ya hizo mbili itafuzu hatua ya fainali, katika mazingira yenye ushindani mkubwa na historia iliyowahi kuziunganisha klabu hizi mbili kwenye matukio ya awali ya mashindano ya visiwani.
Simba inauingia mchezo huu ikiwa na lengo la kupata ushindi na kuendelea na safari yake ya kutafuta taji la kwanza katika msimu huu, huku Mlandege ikilenga kuthibitisha ubora wake kama moja ya timu imara kutoka Zanzibar iliyofanikiwa kufika hatua ya nusu fainali.
Simba vs Mlandege: Nusu fainali ya Kombe la Muungano
Mchezo wa leo umepangwa kuchezwa saa 2:15 usiku kwenye Uwanja wa New Amaan Complex. Ni hatua ya nusu fainali ya pili, ambapo mshindi atakutana na timu itakayopita kutoka nusu fainali ya kwanza.
Simba ilifika hatua hii baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mafunzo ya Zanzibar, bao lililofungwa na Seleman Mwalimu “Gomes” katika dakika ya 53. Mafunzo walitoa upinzani mkubwa katika kipindi cha kwanza, lakini Simba ilifanikiwa kutumia nafasi iliyoipata kipindi cha pili na kupata ushindi huo muhimu.
Kwa upande wa Mlandege, ilitinga nusu fainali baada ya kuifunga Singida Black Stars kwa mabao 2-1 katika hatua ya robo fainali. Matokeo hayo yaliiwezesha kusonga mbele kama timu pekee ya Zanzibar iliyofika hatua hiyo ya juu katika mashindano.
Historia ya Simba dhidi ya Mlandege
Mchezo wa leo unaendelea kujengwa juu ya historia ya mikutano ya awali kati ya timu hizi mbili. Katika Kombe la Mapinduzi 2023, Simba ilitolewa na Mlandege kupitia mikwaju ya penalti baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 za mchezo wa nusu fainali. Mlandege baadaye iliendelea hadi fainali na kutwaa ubingwa.
Msimu uliofuata wa 2024, Mlandege iliendeleza ubora wake dhidi ya Simba kwa ushindi wa bao 1-0 katika fainali ya Kombe la Mapinduzi. Bao hilo lilifungwa na Joseph Akondwanaho, ambaye kwa sasa anaitumikia klabu ya TRA United. Matokeo hayo yanaweka Simba katika nafasi ya kutafuta matokeo chanya katika mchezo wa leo ili kubadili mwenendo wa mikutano ya awali.
Kikosi cha Simba dhidi ya Mlandege
Simba inatarajiwa kuanza na kikosi kifuatacho:
Starting XI – Simba SC
- 28 Abel
- 15 Duchu
- 5 Mligo
- 60 Mbegu
- 23 De Reuck
- 8 Kante
- 27 Bajaber
- 35 Maema
- 34 Mpanzu
- 18 Morice
- 63 Bashiri
Wachezaji wa akiba: Kassali, Kapombe, Toure, Kagoma, Gueye, Chama, Mwalimu, Inno, Oura.
Kikosi cha Mlandege dhidi ya Simba
Mlandege inatarajiwa kuanza na kikosi kifuatacho:
Starting XI – Mlandege
- 31 Baro
- 28 Hashim
- 12 Mbeki (C)
- 23 Nonyem
- 21 Opondo
- 29 Mazni
- 20 Mussa
- 49 Jamal
- 9 Omariy
- 39 Mahmoud
- 14 Kivelege
Wachezaji wa akiba: Alex, Hemil, Masoud, Cahil, Jussa, Ali Khatib, Matola, Macabo.
Fuatilia Hapa Matokeo ya Mlandege VS Simba Leo 26/04/2026
| Mlandege | 0-3 | Simba Sc |
- Goli la kwanza limefungwa na seleman Mwalimu dakika ya 63
- Anicent Oura anatia chuma ya pili kwa Simba Sc dakika ya 76
- 89 Neo Maema anaifungia Simba Goli la 3
Simba na malengo ya msimu
Simba inahitaji ushindi katika mchezo wa leo ili kufanikisha lengo la kufika fainali na kuongeza nafasi ya kutwaa taji la Kombe la Muungano. Klabu hiyo bado inaendelea na harakati za kutafuta mataji katika msimu huu, huku ikiweka kipaumbele katika mashindano ya ndani.
Kabla ya mchezo huu, wachezaji wa Simba walipata muda wa kupumzika na kutembelea maeneo ya vivutio vya utalii Zanzibar, hatua iliyolenga kuongeza utulivu wa kikosi kabla ya maandalizi ya mwisho ya mchezo.
Kocha Steven Barker alieleza kuwa mchezo huu haupaswi kuangaliwa kama wa kulipiza kisasi, bali kama sehemu ya kutimiza malengo ya ushindi na kusonga mbele katika mashindano.
Mlandege na dhamira ya kulinda heshima ya Zanzibar
Mlandege inaingia kwenye mchezo huu ikiwa timu pekee ya Zanzibar iliyofika hatua ya nusu fainali ya Kombe la Muungano. Mafanikio haya yanaiweka katika nafasi ya kuendeleza uwakilishi wa visiwani katika hatua ya juu ya mashindano.
Kocha Hassan Ramadhan alieleza kuwa kikosi chake kimejiandaa kikamilifu kwa mchezo huu na kinaelewa umuhimu wa kupata matokeo chanya dhidi ya Simba. Alisisitiza kuwa mchezo wa mtoano unahitaji umakini katika kila sekunde ya mchezo.
Mapendekezo ya Mhariri:







Leave a Reply