Ratiba ya Fainali Mapinduzi Cup 2026

Ratiba ya Fainali Mapinduzi Cup 2026

Hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Muungano 2026 hatimaye imekamilika kwa ushindani mkubwa ulioshuhudiwa katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, huku timu mbili kubwa zikithibitisha ubora wao na kufuzu rasmi kucheza fainali inayosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini.

Baada ya michezo miwili ya nusu fainali iliyopigwa kwa siku tofauti, sasa pazia limefunguka kuelekea mchezo wa mwisho wa mashindano haya, ambapo Simba SC itakutana na Yanga katika pambano la kumsaka bingwa wa michuano ya kombe la Muungano Msimu wa 2026

Ratiba ya Mchezo wa Fainali Mapinduzi Cup 2026

  • Mechi: Simba SC vs Yanga SC
  • Tarehe: Aprili 29, 2026
  • Saa 02:15 Usiku
  • Uwanja: New Amaan Complex, Zanzibar

Ratiba ya Fainali Mapinduzi Cup 2026

Huu unatarajiwa kuwa mchezo wa ushindani mkubwa ukizingatia historia na ukubwa wa timu hizi mbili kongwe katika soka la Tanzania.

Simba yatinga fainali kwa ushindi mnono

Simba SC imetinga Fainali baada ya kuichapa Mlandege FC mabao 3-0 katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa Aprili 26, 2026.

Mabao ya Simba yalifungwa na Seleman Mwalimu, Ancet Oura na Neo Maema, ambao walionyesha kiwango cha juu na kuhakikisha timu yao inapata ushindi wa kishindo. Ushindi huu pia umeonekana kuwa wa kulipa kisasi kufuatia matokeo ya nyuma ambapo Simba ilikuwa imepoteza michezo miwili mfululizo dhidi ya wapinzani hao kutoka Zanzibar.

Yanga yafuzu Baada ya ushindi dhidi ya Azam FC

Katika nusu fainali ya kwanza iliyochezwa Aprili 25, 2026, Yanga SC iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Azam FC.

Yanga ilianza kwa kasi kubwa, ikipata bao la mapema dakika ya tano kupitia mshambuliaji Prince Dube aliyemalizia pasi ya Allan Okello. Dakika ya 25, Maxi Nzengeli aliongeza bao la pili baada ya kupokea pasi kutoka kwa Dube.

Azam FC ilijaribu kurejea mchezoni na kufanikiwa kupata bao la kufutia machozi dakika ya 77 kupitia Feisal Salum ‘Fei Toto’, lakini juhudi zao hazikutosha kuzuia ushindi wa Yanga.

Ushindi huo uliifanya Yanga kufuzu fainali kwa mara ya pili mfululizo, ikiwa na dhamira ya kutetea taji lake.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. matokeo ya Azam FC vs Yanga SC Leo 25/04/2026
  2. Ratiba ya Nusu Fainali Kombe la Muungano 2026
  3. Timu Zilizofuzu Nusu Fainali Kombe la Muungano 2026
  4. Vilabu Bora Afrika 2026/2027 (CAF Club Ranking)
  5. CAF Rankings 2026: Simba Yaporomoka, Yanga Yaendelea Kung’ara Afrika
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo