Azam Fc Yaambulia Sare ya 0-0 Mbele ya Pamba Jiji
Azam FC imeshindwa kutamba nyumbani, ikilazimishwa sare tasa na Pamba Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara uliochezwa leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, jijini Dar es Salaam.
Hii ni sare ya pili mfululizo kwa Azam FC katika mechi mbili za mwanzo za msimu, kufuatia sare ya 0-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa kwanza Uwanja wa Meja Jenerali Mstaafu Isamuhyo, Mbweni jijini Dar es Salaam.
Pamba Jiji FC nayo inaendeleza wimbi la sare, ikiwa ni sare ya tatu mfululizo katika mechi tatu za mwanzo za msimu, ikijumuisha zile mbili za nyumbani, Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza dhidi ya Tanzania Prisons na Dodoma Jiji FC.
Matokeo haya yanaweka presha kubwa kwa Azam FC katika harakati zao za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.
Je, wanarambaramba wa Chamanzi Dar es salaam wataweza kurejea kwenye mstari wa ushindi katika mechi zijazo? Tueleze mtazamo wako hapa chini kwenye komenti juu kiwango walicho kionesha Azam katika mchezo wa leo
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti