Dortmund Kusubiri Mshindi kati Ya Buyern Dhidi Ya Real Madrid Fainali Klabu bingwa
- Borussia Dortmund imefuzu katika fainali ya kombe la klabu bingwa Ulaya msimu wa mwaka 2024 kwa mara ya tatu katika historia yao, baada ya kuibuka mshindi mnamo mwaka wa 1997 na kumaliza kama Mshindi wa pili mwaka wa 2013 huko Wembley.
Dortmund Kusubiri Mshindi kati Ya Buyern Dhidi Ya Real Madrid Fainali Klabu bingwa
Baada Ya Mtanange mkali kati ya Dortmund na PSG kwenye uwanja wa Parc des Princes, mwisho ni Dortmund ambao wanafuzu hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa . Mats Hummels ndio mfungaji wa goli pekee huku wenyeji PSG wakishindwa kupata njia ya kupita safu ya ulinzi ilioundwa na vijana wa Erin Terzic.
Kipindi cha kwanza cha mchezo wa nusu fainali ya Dortmund dhidi ya PSG kilikwenda sawa kama Dortmund walivyotarajia, huku nyota hatari wa PSG Kylian Mbappé alokua akitokea pembeni mwa uwanja na Gregor Kobel akiwa amefichwa kabisa hadi kukosa la kufanya. PSG wameweza kufanya mashambulizi mbalimbali kupitia mashuti ya mbali ambapo mengi yaliweza kudhibitiwa na golikipa wa Dortmund na mengine ma nne yaliishia kugongo nguzo za gori.
Kipindi cha pili kilikuwa cha mchezo kilianza uku dortmund ikiwa na ukuta mkubwa na kutegemea mashambulizi ya kushtukiza, ambapo waliweza kupata goli baada ya Hummels kuunganisha mpira wa kona kwa kichwa.
Baada ya matokeo haya, Dortmund sasa anasubili mshindi kati ya Real Madrid na Bayern Munich kucheza mchezo wa fainali ya Klabu bingwa ulaya 2024 utakao chezeka uwanja wa Wembley mnamo Juni 1. Mchezo wa marudiano kati ya Real Madrid na Bayern Munich wa nusu fainali uta chezeka Jumatano 08 2024.
Machaguo ya Mhariri
- Borussia Dortmund Yiondoa PSG Katika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Ulaya 2024
- Hiki Apa Kikosi Cha Taifa Stars Kitakacho Cheza Na Sudan Mechi za Kirafiki 2024
- Upambanaji na Kujiamini: Sababu za Kupanda kwa Thamani ya Kibu D
- Simba SC Yasaka Kocha Mpya Mwenye Uzoefu wa CAF
- Paul Pogba Ageukia Filamu Baada ya Kufungiwa Soka kwa Miaka Minne
Weka Komenti