Kikosi cha Simba vs Namungo leo 19/04/2026
Mnyama Simba SC anashuka dimbani leo akiwa na dhamira ya kusaka alama tatu muhimu ugenini, katika pambano dhidi ya Namungo FC linalotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ndani ya NBC Premier League. Mchezo huu unavutia macho ya mashabiki wengi kutokana na historia ya timu hizi mbili pamoja na nafasi zao tofauti kwenye msimamo wa ligi.
Mchezo utachezwa saa ngapi na wapi?
Kwa mujibu wa ratiba rasmi, mchezo wa Kikosi cha Simba vs Namungo leo 19/04/2026 utapigwa:
- Tarehe: 19 Aprili 2026
- Muda: Saa 10:00 jioni (16:00 HRS)
- Uwanja: Majaliwa Stadium, Ruangwa
Namungo FC watakuwa wenyeji wakimkaribisha Simba SC katika dimba lao la nyumbani, huku mashabiki wakitarajiwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia pambano hilo. Mchezo pia utarushwa mubashara kupitia AzamSports1HD.
Hali ya timu kabla ya mchezo
Simba SC wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 39 baada ya kucheza mechi 18. Kwa upande wa Namungo FC, wao wanashika nafasi ya 10 wakiwa na pointi 22 kutoka mechi hizo hizo 18.
Tofauti hii ya pointi inaonyesha wazi namna timu hizi zilivyokuwa na mwenendo tofauti msimu huu, huku Simba wakionekana kuwa na uthabiti zaidi ukilinganisha na Namungo.
Kikosi cha Simba vs Namungo leo 19/04/2026
Kikosi cha Simba leo kitakuwa na jukumu la kuzisaka pointi tatu muhimu kwa hali na mali ili kuendelea kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kupambania ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC. Mchezo huu wa ugenini dhidi ya Namungo FC unakuja katika kipindi ambacho ushindani wa ligi umeendelea kuwa mkubwa, hivyo kila alama ina uzito mkubwa kwa timu zinazowania nafasi za juu.
Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker, anatarajiwa kutangaza kikosi chake majira ya saa 9 mchana kuelekea mchezo huo wa saa 10:00 jioni. Mashabiki wa Simba wanasubiri kwa hamu kuona majina ya wachezaji watakaoanza, wakitarajia kikosi chenye uwezo wa kuanza kwa kasi na kuhakikisha wanapata mabao ya mapema ili kudhibiti mchezo.
Kutokana na mwenendo mzuri wa Simba SC katika mechi za hivi karibuni, ambapo hawajapoteza katika michezo mitano iliyopita, matarajio ni kwamba kocha ataendelea kuwaamini wachezaji waliopo kwenye kiwango kizuri. Uwepo wa mshambuliaji Seleman Mwalimu, ambaye tayari ana mabao 6, unatarajiwa kuwa sehemu muhimu ya kikosi kitakachotumika leo.
Hiki apa kikosi cha simba leo dhidi ya namungo
Kwa upande wa Namungo FC, nao watakuwa na kikosi chenye lengo la kulinda uwanja wao wa nyumbani Majaliwa Stadium. Mshambuliaji wao kinara Fabrice Ngoyi mwenye mabao 8 anatarajiwa kuwa tishio kubwa kwa safu ya ulinzi ya Simba SC.
Hata hivyo, kutokana na rekodi nzuri ya Simba dhidi ya Namungo, presha kubwa ipo kwa wenyeji kujaribu kubadilisha historia hiyo, huku Simba wakihitaji kuendelea kuonyesha ubora wao ili kuondoka na ushindi muhimu wa ugenini.
Rekodi ya makabiliano (Head-to-Head)
Historia inaipa nguvu Simba SC katika mechi dhidi ya Namungo FC:
- Jumla ya mechi: 13
- Simba SC wameshinda: 8
- Sare: 5
- Namungo FC hawajawahi kushinda
Katika upande wa mabao:
- Simba SC wamefunga mabao 27
- Namungo FC wamefunga mabao 9
Mara ya mwisho walipokutana msimu huu, Simba walishinda kwa mabao 3-0 katika mchezo uliochezwa Dar es Salaam Oktoba 2025.
Matokeo ya hivi karibuni yanaendelea kuonyesha ubora wa Simba, wakiwa na ushindi wa 3-0 mara kadhaa, huku Namungo wakifanikiwa kupata sare chache tu kama 2-2 na 1-1.
Kauli za makocha kabla ya mchezo
Kocha Mkuu wa Namungo FC, Juma Mgunda, alieleza kuwa maandalizi ya timu yake yako tayari na wapo tayari kwa changamoto:
“Maandalizi yapo tayari kuelekea mchezo wetu dhidi ya Simba SC, tunatambua utakuwa mchezo wenye ushindani tukiwa nyumbani, mashabiki wajitokeze kwa ajili ya kutushangalia.”
Kwa upande wa Simba SC, Kocha Mkuu Steve Barker alisisitiza umuhimu wa maandalizi:
“Tumefanya maandalizi mazuri tunatambua utakuwa ni mchezo mgumu. Tunahitaji kucheza vizuri na kupata matokeo mazuri.”
Mapendekezo ya Mhariri:








Leave a Reply