Matokeo ya Namungo vs Simba leo 19/04/2026
Mnyama Simba SC anashuka dimbani leo kusaka alama tatu muhimu ugenini dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa NBC Premier League utakaopigwa Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa. Ni mechi inayobeba uzito mkubwa kwa pande zote mbili, huku Simba wakihitaji kuendelea kusalia kwenye mbio za juu za ligi na Namungo wakisaka ushindi muhimu mbele ya mashabiki wao.
Taarifa za Mchezo
- Namungo FC vs Simba SC
- Tarehe: 19 Aprili 2026
- Muda: Saa 10:00 jioni (16:00 HRS)
- Uwanja: Majaliwa Stadium, Ruangwa
- Mubashara: AzamSports1HD
Simba SC Wameanza na Kikosi Gani?
Simba SC wameanza mchezo huu wakiwa na kikosi chenye mchanganyiko wa uzoefu, uimara wa ulinzi na kasi mbele ya lango. Kikosi cha kwanza kilichotangazwa ni kama ifuatavyo:
Starting XI ya Simba SC
39 – Kassali
12 – Kapombe (C)
5 – Mligo
25 – Toure
23 – De Reuck
21 – Kagoma
7 – Gueye
17 – Chama
40 – Mwalimu
10 – Inno
20 – Oura
Substitutes: Abel, Duchu, Mbegu, Semfuko, Chasambi, Neo, Bashiri, Baraka, Morice, Mpanzu.
Kikosi hiki kinaonyesha Simba wakiwa na mpango wa kuingia kwa kasi na nidhamu, hasa kwa kuzingatia umuhimu wa pointi tatu kwenye mchezo wa leo.
Matokeo ya Namungo vs Simba leo 19/04/2026
| Namungo | VS | Simba Sc |
Msimamo wa Timu Kabla ya Mechi
Simba SC wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kwa pointi 39 baada ya kucheza mechi 18. Namungo FC wao wako nafasi ya 10 kwa pointi 22, nao pia wakiwa na idadi sawa ya michezo.
Takwimu hizi zinaonyesha tofauti ya ubora na uthabiti uliopo kati ya timu hizo msimu huu, ingawa mchezo wa leo unaweza kuandika sura mpya kutokana na uzito wa uwanja wa nyumbani kwa Namungo.
Historia Ya Michezo ya Namungo vs Simba Sc
Rekodi ya michezo ya awali baina ya timu hizi inaendelea kuipa Simba SC faida kubwa.
Katika mechi 13 zilizopita:
- Simba SC wameshinda mara 8
- Sare ni mara 5
- Namungo FC hawajawahi kupata ushindi
Kwa upande wa mabao, Simba wamefunga jumla ya 27, huku Namungo wakifunga 9 pekee. Takwimu hizo zinaeleza wazi namna Simba walivyo na nafasi kubwa kwenye historia ya mechi hizi.
Mchezo wa kwanza baina yao msimu huu uliisha kwa Simba kushinda 3-0 jijini Dar es Salaam, matokeo yaliyoongeza presha kwa Namungo kuelekea mchezo wa leo.
Fomu ya Hivi Karibuni
Simba SC wanaingia kwenye mtanange huu wakiwa katika mwenendo mzuri. Katika michezo yao mitano ya mwisho, wamepata:
- Ushindi 3
- Sare 2
Namungo FC wao wamekuwa wakipambana kutafuta uthabiti zaidi, wakifanikiwa kupata ushindi mmoja tu katika michezo yao mitano ya mwisho.
Hii inaipa Simba nafasi ya kuingia uwanjani wakiwa na morali ya juu, lakini pia Namungo watajaribu kutumia uwanja wao wa nyumbani kugeuza mambo.
Kauli za Makocha
Kocha Mkuu wa Namungo FC, Juma Mgunda, alisema maandalizi yamekamilika na timu yake iko tayari kwa mchezo huu mgumu:
“Maandalizi yapo tayari kuelekea mchezo wetu dhidi ya Simba SC, tunatambua utakuwa mchezo wenye ushindani tukiwa nyumbani, mashabiki wajitokeze kwa ajili ya kutushangalia.”
Kwa upande wa Simba SC, Kocha Mkuu Steve Barker alieleza kuwa wamejipanga vizuri na wanajua wanakutana na mpinzani mgumu:
“Tumefanya maandalizi mazuri tunatambua utakuwa ni mchezo mgumu. Tunahitaji kucheza vizuri na kupata matokeo mazuri.”
Uchambuzi wa Mchezo
Kwa kuangalia takwimu, historia na ubora wa vikosi, Simba SC wanaingia kama wanaopigiwa hesabu kubwa ya kuondoka na ushindi. Hata hivyo, soka halitabiriki kila mara, na Namungo FC wakiwa nyumbani watajaribu kupambana kwa nguvu zote ili kuibua matokeo tofauti.
Mchezo huu unatarajiwa kuwa wa ushindani mkubwa kutokana na hali ya kila timu kwenye msimamo wa ligi, pamoja na hamu ya kupata pointi tatu muhimu katika hatua hii ya msimu.
Mapendekezo ya Mhariri:








Leave a Reply