Kikosi cha Yanga Vs Vitalo Leo 24/08/2024 | Kikosi cha Yanga Leo Dhidi ya Vital’o Klabu Bingwa
Klabu ya Yanga SC leo itaikaribisha Vital’O katika mchezo wa marudiano wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika CAF kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamanzi leo Agosti 24, majira ya saa moja usiku. Huu ni mchezo muhimu kwa Yanga, ambao walipata ushindi wa kishindo wa mabao 4-0 katika mechi ya awali dhidi ya mabingwa hao wa Burundi, Vital’O.
Katika mchezo wa leo, Yanga SC inahitaji kuhakikisha wanadumisha kasi yao na kupata matokeo mazuri ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu kwa raundi inayofuata ya michuano hii ya kimataifa. Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi, amesisitiza kwamba licha ya ushindi mzuri kwenye mechi ya awali, bado wana kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha wanavuka salama hatua hii.
Yanga itaingia uwanjani ikiwa na kikosi chao kamili, ambacho kimejizatiti kutafuta ushindi mwingine mnono. Gamondi amethibitisha kuwa atashusha kikosi chenye nguvu, akilenga kuandikisha ushindi mkubwa zaidi.
Licha ya kuongoza kwa mabao 4-0, Gamondi anaamini wapinzani wao watakuja na mbinu mpya, hivyo wachezaji wa Yanga wanatakiwa kuwa makini na kuhakikisha wanadhibiti mchezo kwa dakika zote 90.
Mbali na ushindi, Yanga pia inatamani kuendelea kuvuna zawadi nono kutoka kwa Rais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, ambaye aliahidi kutoa Sh 5 milioni kwa kila bao litakalofungwa na timu za Tanzania katika michuano ya kimataifa. Kwa ushindi wa mabao 4-0, Yanga tayari imevuna Sh 20 milioni, na leo wanapanga kuongeza zaidi kiasi hicho.
Kwa upande wao, Vital’O wanakabiliwa na changamoto kubwa baada ya kupoteza kwa mabao mengi kwenye mechi ya awali. Hata hivyo, kocha wao, Parris Sahabo, amedokeza kuwa timu yake haitajiweka kwenye mkakati wa kujilinda tu, bali watatafuta mabao ya haraka ili kuweka presha kwa Yanga. Sahabo ameeleza kuwa wanatambua ubora wa Yanga, lakini wana matumaini ya kufanya tofauti kwenye mechi hii ili kuwashangaza mashabiki na kufungua milango ya mafanikio zaidi kwa wachezaji wao vijana.
Kikosi cha Yanga Vs Vitalo Leo 24/08/2024
Kikosi cha Yanga Leo dhidi ya Vitalo kinatarajiwa kutangazwa lisaa limoja kabla ya mchezo kuanza, hivyo endelea kutembelea ukurasa huu kupata taarifa kamili na orodha ya wachezaji wote watakao unda kikosi cha Yanga leo.
Mashabiki wa Yanga wanatarajiwa kufurika uwanjani leo, wakiwa na matumaini ya kuona timu yao ikipata ushindi mwingine mkubwa na kufuzu kwa raundi inayofuata ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika CAF. Kwa upande wa Vital’O, ingawa wanakabiliwa na kibarua kigumu, wana matumaini ya kupambana kwa uwezo wao wote na kuonyesha kwamba wao ni wapinzani wa kweli.
Kwa mashabiki wa soka, ni mechi inayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, ambapo Yanga SC inatazamia kuongeza nguvu na kuendelea kupeperusha bendera ya Tanzania kwenye michuano ya kimataifa.
Mapenekezo ya Mhariri:
- Msimamo NBC Premier league 2024/2025 | Ligi Kuu Bara
- Usajili wa Chelsea 2024/2025
- PSG Hatarini Kufungiwa Kushiriki UEFA Baada ya Mbappe Kudai €55M za Mishahara na Marupurupu
- Ronaldo Azindua Rasmi Chaneli ya YouTube
- Tabora United Yaahidi Kulipiza Kisasi kwa Namungo Mchezo Ujao wa Ligi Kuu
- Ateba Tayari Kutinga Uwanjani: Simba SC vs Fountain Gate
Weka Komenti