Matokeo ya Simba Leo VS Azam Fc | Matokeo ya Azam fc Vs Simba Leo 26/09/2024
Usiku wa leo, tarehe 26 Septemba 2024, Simba SC inakutana na Azam FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2024/2025, itakayofanyika katika dimba la New Amaan, Zanzibar. Mechi hii imekuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki kutokana na historia na ushindani uliopo baina ya timu hizi mbili tangu Azam ilipopanda daraja mwaka 2008.
Hii ni mechi ambayo itatoa taswira ya ushindani wa msimu wa 2024/2025, huku kila timu ikiwa chini ya uongozi wa makocha wapya na wakiwa na vikosi vilivyoboreshwa kwa wachezaji wapya wenye uwezo wa kubadili matokeo. Simba, chini ya kocha wake Fadlu Davids, na Azam, inayoongozwa na Mmorocco Rachid Taoussi, zitaingia uwanjani na mikakati madhubuti kuhakikisha zinaibuka na ushindi.
Matokeo ya Azam fc Vs Simba Leo 26/09/2024
Azam Fc | VS | Simba Sc |
- 🚨 M A T C H D A Y 🚨
- Azam Fc🆚 Simba SC
- 🏆 NBC Premier League
- ®️ Round 5
- 🏟 New Amaan Complex
- 🕰 8.30 PM (E.A.T)
Kikosi cha Simba Leo VS Azam Fc
Katika mechi ya leo, Wekundu wa Msimbazi Simba wanatarajiwa kuanza na kikosi chenye nguvu zaidi, kikiongozwa na wachezaji waliopo kwenye kiwango bora. Mchezaji tegemeo, Debora Fernandez na Valentino Mashaka, ambaye alisajiliwa kutoka Geita Gold, ameanza msimu kwa kiwango cha hali ya juu akiwa ameshafanikiwa kutia kambani goli mbili. Jean Charles Ahua, kutoka Ivory Coast, naye anatarajiwa kutoa mchango mkubwa baada ya kuonyesha uwezo wake wa kutoa pasi za mabao tatu msimu huu.
Simba itawategemea pia Lionel Ateba na Edwin Balua, ambao wamesajiliwa msimu huu kuimarisha safu ya ushambuliaji, huku Steven Mukwala na Joshua Mutale wakitarajiwa kuchangia zaidi katika mashambulizi dhidi ya ngome ya Azam.
Hiki Apa Kikosi cha Simba Dhidi ya Azam Fc
Hiki apa kikosi cha Azam Leo Dhidi ya Simba
Historia na Takwimu za Mechi za Azam Vs Simba Zilizopita
Katika michezo 32 ya ligi iliyopita baina ya Simba na Azam, Simba imeonekana kuwa na ubabe zaidi. Wamefanikiwa kushinda michezo 14 dhidi ya sita ya Azam, huku michezo 12 ikimalizika kwa sare. Simba pia imekuwa na mafanikio makubwa zaidi katika kufunga mabao, ikiwa na mabao 44 dhidi ya 29 ya Azam.
Katika pambano la mwisho walipokutana kwenye Ligi Kuu msimu uliopita, Simba ilishinda mabao 3-0 dhidi ya Azam, na hivyo leo Azam FC itakuwa na kibarua cha kulipiza kisasi. Lakini haijawa kazi rahisi kwa timu zote, kwani kila mmoja ana rekodi ya kutofanya vizuri ugenini dhidi ya mwenzake. Kwa Simba, wakiwa ugenini, wamepoteza mechi mbili na kutoka sare saba, huku Azam ikiwa na rekodi ya kupoteza michezo saba nyumbani.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Kikosi cha Azam Vs Simba Leo 26/09/2024
- Azam Vs Simba Leo 26/09/2024 Saa Ngapi?
- Matokeo Kengold Vs Yanga Sc Leo 25/09/2024
- Kikosi cha Yanga Vs Kengold Leo 25 September 2024
- Fadlu David na Simba SC Wamejipanga Vyema Kukabiliana na Azam FC Kesho
- Kengold Wakijichanganya Tunawapiga Nyingi, Gamondi Atoa Onyo
Weka Komenti