Matokeo ya Mechi ya Tanzania Taifa Stars Vs Guinea Leo

Matokeo ya Mechi ya Tanzania Taifa Stars Vs Guinea Leo 10 September 2024 | Matokeo Tanzania Vs Guinea Kufuzu AFCON 2025

Leo, timu ya Taifa Stars ya Tanzania inakabiliana na Guinea katika mechi muhimu ya kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025. Mchezo huu unachezwa kwenye uwanja wa Charles Konan Banny, Yamoussoukro, nchini Ivory Coast. Huu ni mchezo wa pili kwa Taifa Stars katika hatua ya makundi, baada ya mechi ya kwanza dhidi ya Ethiopia kumalizika kwa sare tasa nyumbani.

Safu ya ushambuliaji ya Taifa Stars leo itaongozwa na washambuliaji mahiri, Wazir Junior na Cyprian Kachwele. Hawa ni wachezaji wenye uwezo wa kupeleka mashambulizi kwa kasi, wakisaidiana na kiungo mshambuliaji, Simon Msuva.

Katika mechi zilizopita, changamoto kubwa kwa Taifa Stars imekuwa ni kutumia nafasi zinazotengenezwa, huku wakikosa umakini kwenye kufunga licha ya kufanya mashambulizi mengi.

Kwa upande wa Guinea, timu hiyo inatoka katika kipigo cha 1-0 dhidi ya DR Congo katika mchezo wa awali. Hii inaifanya Guinea kuingia uwanjani leo ikiwa na presha ya kurejesha heshima na kurekebisha rekodi yao mbovu ya kufungwa mechi mbili mfululizo.

Kwenye michezo iliyopita ya mwezi Machi na Juni mwaka huu, Guinea ilipata ushindi wa mechi tatu mfululizo, lakini sasa inakabiliwa na changamoto ya kudumisha ubora huo.

Matokeo ya Mechi ya Tanzania Taifa Stars Vs Guinea Leo – 10 Septemba 2024

Guinea 1-2 Tanzania
  • 88′ Mudathir Yahya Anaifungia Tanzania Goli la Pili
  • 61′ 1 – 1 Goli kwa Tanzania (Feisali Atasawazisha).
  • 57′ 1 – 0 Guinea Wanapata Goli la kutangulia.
  • 2T Kipindi cha pili kinaanza.
  • HT: Mapumziko ya Kipindi cha Kwanza – 0 : 0
  • 36′ Mchezaji wa Tanzania ameonyeshwa kadi ya njano.
  • 25′ Mchezaji wa Tanzania ameonyeshwa kadi ya njano.
  • 1T Kipindi cha kwanza kinaanza.”

Matokeo ya Mechi ya Tanzania Taifa Stars Vs Guinea Leo

Kikosi cha Taifa Stars Vs Guinea Leo

Kikosi cha Taznania Taifa stas Vs Guinea leo katika mchezo wa kufuzu AFCON 2025

  1. Ally Salum (Gk)
  2. Lusijo Mwaikenda
  3. Mohamed Hussein ©
  4. Dickson Job
  5. Ibrahim Abdilla
  6. Novatus Dismas
  7. Edwin Balama
  8. Mudathir Yahya
  9. Feisal Salum
  10. Walid Junior

Kocha: Heemed Suleiman

Wachezaji wa Ziada: 10. Mohammed Issa, 17. Yahya Zayd, 22. Abel Solomon

Rekodi za Taifa Stars Katika Mwaka 2024

Kwa Taifa Stars, mwaka 2024 umekuwa na changamoto kadhaa, ambapo timu imeshinda mechi tatu tu kati ya 11 zilizochezwa hadi sasa, ikiwa ni za kirafiki na mashindano rasmi. Ushindi wa hivi karibuni dhidi ya Zambia kwenye mechi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 ulileta matumaini kwa mashabiki, ambapo Wazir Junior alifunga bao pekee mapema dakika ya tano.

Hata hivyo, tatizo la kumalizia mashambulizi limekuwa likijirudia katika mechi kadhaa, na leo benchi la ufundi chini ya kocha Hemed Morocco linatarajiwa kufanya marekebisho kuhakikisha nafasi zinatumiwa ipasavyo.

Ulinzi Imara wa Taifa Stars

Licha ya changamoto za kufunga mabao, safu ya ulinzi ya Taifa Stars imeonyesha uimara, ikiwa imefanikiwa kupata clean sheet sita katika mechi 11 zilizopita. Beki Novatus Dismas, ambaye alifunga bao muhimu katika mechi za awali, atakuwa na jukumu kubwa leo kuhakikisha kuwa wanazuia mashambulizi ya Guinea.

Historia ya Mikutano ya Taifa Stars VS Guinea

Mechi ya mwisho kati ya Tanzania na Guinea ilichezwa Januari 2021 katika michuano ya CHAN nchini Cameroon, ambapo timu hizo zilitoka sare ya 2-2. Katika kikosi cha leo, ni wachezaji wachache pekee waliobaki kutoka kikosi hicho cha zamani, akiwemo Bakari Mwamnyeto na Feisal Salum. Hii inaashiria mabadiliko makubwa kwenye timu ya Taifa Stars, huku kocha Morocco akilenga kujenga kikosi kipya chenye nguvu.

Maandalizi ya Timu na Kauli za Kocha

Kocha Hemed Morocco amesema anaelewa changamoto ya kucheza ugenini dhidi ya Guinea, hasa kwa kuwa wenyeji watakuwa na hamasa kubwa ya kushinda. Hata hivyo, Morocco ana imani na wachezaji wake na amesema maandalizi ya timu yamekuwa mazuri.

“Tunajua mchezo huu utakuwa mgumu, lakini tumejiandaa vyema. Suala la kutengeneza nafasi ni muhimu, lakini la kuzitumia nafasi hizo ni jambo la msingi zaidi, na nadhani leo tutakuwa na mafanikio mazuri katika hilo,” alisema Morocco.

Msimamo wa Kundi H Kufuzu AFCON 2025

Katika kundi H la kufuzu AFCON 2025, timu zinazoshiriki ni Tanzania (Taifa Stars), Guinea, DR Congo, na Ethiopia. Kabla ya mchezo wa leo, DR Congo inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi tatu baada ya ushindi dhidi ya Guinea, huku Ethiopia ikiwa na pointi moja baada ya sare na Tanzania. Guinea bado haina pointi baada ya kupoteza mechi zake mbili za mwanzo.

Taifa Stars inahitaji ushindi leo ili kuweka hai matumaini ya kufuzu kwenye michuano ya AFCON 2025, itakayofanyika nchini Morocco kuanzia Desemba 21, 2025 hadi Januari 18, 2026.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Kikosi cha Tanzania Taifa Stars vs Guinea 10 September 2024
  2. Matokeo ya Guinea vs Tanzania Taifa Stars Leo 10/09/2024
  3. Mshambuliaji wa Namungo Fabrice Ngoy Aweka Malengo Mapya
  4. Ratiba ya Mechi za Leo 09 September 2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo