Matokeo ya Simba Vs Al Ahli Tripoli Leo 22/09/2024 | Matokeo ya Simba Leo Vs Al Ahli Tripoli
Baada ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania, Yanga SC, kufuzu hatua ya makundi ya Klabu Bingwa Afrika kwa staili ya aina yake, leo Simba SC watashuka dimbani kupambania nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika. Simba SC watawakaribisha Al Ahli Tripoli kwenye dimba la Benjamin Mkapa, majira ya saa kumi kamili.
Mchezo huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na ubora wa timu zote, ambao umeonekana kwenye mchezo wa kwanza, uliomalizika kwa sare ya bila kufungana.
Simba SC wanatupa karata muhimu leo wakiwa na lengo la kufuzu hatua ya makundi ya makombe ya CAF kwa mara ya tano mfululizo. Miaka ya nyuma, klabu hiyo iliweza kufikia hatua hiyo katika misimu ya 2020/2021, 2021/2022, 2022/2023, na 2023/2024.
Ushindi wowote leo utaihakikishia Simba tiketi ya kuingia makundi, jambo ambalo kocha wa Simba, Fadlu Davids, amesisitiza kuwa ni lazima kutekeleza. Simba wanapaswa kuimarisha safu yao ya ushambuliaji, kuhakikisha wanatumia nafasi vizuri kufanikisha malengo hayo.
Matokeo ya Simba Vs Al Ahli Tripoli Leo 22/09/2024
Simba Sc | VS | AL Ahli Tripoli |
- 🏆 #Kombe la Shirikisho CAF
- ⚽️ Young Africans SC🆚CBE FC
- 📆 22.09.2024
- 🏟 Benjamin Mkapa
- 🕖 04:00PM(EAT)
Katika mchezo wa kwanza dhidi ya Al Ahli, Simba walikosa ufanisi katika kutengeneza nafasi za mabao, na walishindwa hata kupiga shuti moja lililolenga lango. Kwa upande wa mawinga wa Simba, Joshua Mutale na Edwin Balua, walionekana kuwa na changamoto ya kupoteza mipira mara kwa mara. Katika mchezo wa leo, wanatakiwa kuimarisha kiwango chao ili kuhakikisha wanazalisha mashambulizi ya kutosha na kusaidia timu kufikia lengo la ushindi.
Ngome ya ulinzi ya Simba imeonekana kuwa thabiti msimu huu, ikiwa imeruhusu bao moja tu katika mechi tano za mashindano walizocheza. Tangu kuanza kwa msimu huu, Simba imeweka rekodi ya kuwa na safu ngumu ya ulinzi, jambo linaloleta matumaini makubwa kwa mashabiki wa timu hiyo. Kwa upande wa Al Ahli Tripoli, wao wameruhusu mabao matatu katika mechi tano zilizopita, jambo linalowapa Simba nafasi ya kutumia mwanya huo kupata ushindi.
Kocha Fadlu Davids amesisitiza kuwa lengo la leo ni kushinda na kufuzu hatua ya makundi. Alisema: “Tunapaswa kucheza kwa umakini mkubwa na kuhakikisha haturuhusu bao. Kama tukiruhusu bao, tunahitaji kufunga mawili ili kuendelea mbele.”
Fadlu pia aliwahimiza mashabiki wa Simba kuipa timu yao sapoti bila kufanya vitendo vya fujo, hasa baada ya vurugu zilizotokea kwenye mchezo wa awali nchini Libya.
Mashabiki wa Simba wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi leo kwenye dimba la Benjamin Mkapa, wakitarajia ushindi wa kishindo. Simba SC wameonesha kuwa na rekodi nzuri wanapocheza nyumbani kwenye michezo ya kimataifa, ambapo katika michezo kumi iliyopita ya kimataifa wakiwa nyumbani, wameibuka na ushindi mara sita.
Kikosi cCha Simba Leo Vs Al Ahli
- Camara (40)
- Kapombe (12)
- Hussein (15) – Captain
- Hamza (14)
- Che Malone (20)
- Kagoma (21)
- Kibu (38)
- Fernandes (17)
- Ateba (13)
- Ahoua (10)
- Mutale (26)
Wachezaji wa Ziada: Ally, Kijili, Nouma, Chamou, Ngoma, Okeejepha, Awesu, Muukwaala & Balua
Al Ahli Tripoli: Hatari Ugenini
Pamoja na changamoto zinazowakabili, Al Ahli Tripoli si timu ya kubezwa, hasa wanapokuwa ugenini. Katika mechi zao 10 za kimataifa zilizopita ugenini, Al Ahli wameibuka na ushindi mara nne, sare mbili, na kupoteza michezo minne. Hivyo Simba wanapaswa kuwa makini ili kuhakikisha wanadhibiti mashambulizi ya wapinzani wao na kuepuka adhabu yoyote.
Mchezo Utachezeshwa na Mwamuzi Abdoulaye Manet
Mchezo wa leo utaongozwa na mwamuzi Abdoulaye Manet kutoka Guinea, akisaidiwa na wasaidizi wake Sidiki Sidibe, Yamoussa Sylla, na Bangaly Konate, wote kutoka Guinea. Huu ni mchezo wa kwanza kwa Manet kuchezesha michuano ya vilabu Afrika, lakini kwa Simba na mashabiki wake, wanategemea haki itatendeka katika uwanja.
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti