Yanga Sc Wafuzu Makundi Klabu Bingwa Kibabe
labu ya Yanga SC, maarufu kama “Wana Jangwani au Timu ya Wananchi,” wameendelea kuthibitisha ubora wao katika uwanja wa soka la Afrika baada ya kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa msimu wa pili mfululizo.
Ushindi wa kishindo dhidi ya CBE SA kutoka Ethiopia uliofanyika visiwani Zanzibar umeweka rekodi ya pekee kwa klabu hiyo, ikiwa ni hatua nyingine kubwa katika historia yao ya ushiriki wa michuano ya kimataifa ya Klabu Bingwa.
Katika mchezo wa marudiano uliofanyika jana tarehe 21 septemba usiku, Yanga ilikamilisha ushindi wa jumla wa mabao 6-0 dhidi ya CBE. Bao la ugenini lililopatikana katika mchezo wa kwanza nchini Ethiopia liliweka msingi mzuri wa ushindi huu, huku timu ikihitaji sare tu ili kufuzu. Baada ya mchezo wa jana wa marudiano kumalizika kwa 6-0, na hivyo Yanga kuhitimisha safari yao ya kufuzu hatua ya makundi kwa jumla ya goli 7-0 kwa mara nyingine tena.
Kikosi Bora na Kiu ya Mabao
Rekodi ya Yanga katika mashindano ya msimu huu imeendelea kuwa ya kuvutia. Katika mechi zao sita zilizopita za mashindano tofauti, Wana Jangwani wamefunga jumla ya mabao 18 huku wakiruhusu bao moja tu.
Kikosi kinachoongozwa na kocha Miguel Gamondi kimeonyesha kiwango bora, huku wachezaji kama Prince Dube, Maxi Nzengeli, Stephane Aziz KI, na Kennedy Musonda wakiendeleza makali yao katika safu ya ushambuliaji.
Kocha Gamondi, ambaye aliongoza Yanga kutetea mataji yao ya Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho msimu uliopita, amekuwa na kauli mbiu ya kushambulia kwa nguvu na kutumia nafasi vyema. Akizungumza na vyombo vya habari kabla ya mechi dhidi ya CBE, Gamondi alisema, “Malengo yetu ni kuhakikisha kila nafasi tunayoipata inakuwa bao, na timu yetu inakuwa bora zaidi kadiri muda unavyosonga.”
Yanga na Rekodi ya Mabao
Msimu huu, Yanga imeanza kwa moto mkali. Baada ya kushinda Ngao ya Jamii kwa kuifunga Azam FC 4-1, waliendeleza ubabe wao katika Ligi ya Mabingwa kwa kuichapa Vital’O ya Burundi jumla ya mabao 10-0 katika mechi mbili. Ushindi wa 1-0 dhidi ya CBE nchini Ethiopia uliongeza imani ya kufuzu, na sasa wamefikia malengo yao kwa kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Yanga pia imeweka rekodi ya mabao mengi dhidi ya timu pinzani msimu uliopita, ikiwemo ushindi wa 5-1 dhidi ya Simba SC, 5-0 dhidi ya KMC, na 5-1 dhidi ya JKT Tanzania. Wachezaji kama Aziz KI, aliyeongoza orodha ya wafungaji wa Yanga msimu uliopita kwa mabao 21, wameendelea kuwa tishio kwa wapinzani.
Kocha Gamondi na Malengo ya Msimu Huu
Gamondi ameweka wazi kuwa malengo ya Yanga msimu huu ni makubwa zaidi.
Baada ya kuwashinda wapinzani wao wa jadi, Simba SC, kwa mara kadhaa msimu uliopita, Gamondi anataka kuhakikisha Yanga inaendelea kudhibiti soka la ndani na kufikia mafanikio makubwa kimataifa.
“Msimu huu ni wa kuchukua kila nafasi kwa umakini mkubwa. Tunataka kuona wachezaji wetu wanatumia kila nafasi kuwa bao, na hilo litatusaidia katika mechi zijazo za kimataifa na ligi ya ndani,” alisema Gamondi baada ya ushindi dhidi ya CBE.
Hatua Inayofuata: Ligi ya Mabingwa na Ligi Kuu
Baada ya kufuzu makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga sasa itarudi kwenye majukumu ya Ligi Kuu Bara ambapo itavaana na KenGold jijini Mbeya. Mchezo huo utakuwa muhimu kwa kocha Gamondi kuhakikisha kikosi kinaendelea kuwa kwenye ubora wake kabla ya hatua ya makundi kuanza. KenGold, ambayo imepanda daraja msimu huu, haijashinda mechi yoyote katika Ligi Kuu, hivyo Yanga ina nafasi nzuri ya kuendeleza rekodi yao nzuri ya ushindi.
Yanga pia itaangazia kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji na kuimarisha safu ya ulinzi ili kuhakikisha wanapiga hatua kubwa zaidi katika michuano ya kimataifa. Matarajio ya mashabiki wa Yanga ni kuona timu yao ikifika mbali zaidi kuliko msimu uliopita ambapo walitolewa kwenye hatua ya robo fainali.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Kikosi cha Simba Vs Al Ahli Tripoli Leo 22/09/2024
- Simba VS AL Ahli Tripoli Leo 22/09/2024 Saa Ngapi
- Timu zilizofuzu Makundi Klabu Bingwa Afrika 2024/2025
- Matokeo ya Yanga Vs CBE SA Leo 21 September 2024
- Yanga Vs CBE SA Leo 21/09/2024 Saa Ngapi
- Ley Matampi Ajitoa Mapema Mbio za Kipa Bora
- Picha za Jezi Mpya za Pamba Fc 2024/2025
Weka Komenti