Mlandege vs Simba Leo 26/04/2026 Saa Ngapi?

Mlandege vs Simba Leo 26/04/2026 Saa Ngapi?

Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, wanatarajiwa kushuka dimbani leo wakiwa na lengo la kusaka tiketi ya fainali ya Kombe la Muungano 2026, wakikutana uso kwa uso na mabingwa wa Zanzibar, Mlandege, katika pambano linalotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Mchezo huu wa nusu fainali ya pili unatajwa kuwa miongoni mwa michezo yenye mvuto mkubwa kutokana na historia na ubora wa timu hizi mbili.

Mlandege vs Simba Leo Saa Ngapi?

Kwa mujibu wa ratiba rasmi ya mashindano, mchezo kati ya Mlandege dhidi ya Simba utachezwa leo tarehe 26 Aprili 2026, saa 2:15 usiku, katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Mlandege vs Simba Leo 26/04/2026 Saa Ngapi?

Safari ya Timu Hadi Nusu Fainali

Timu zote mbili zinaingia kwenye mchezo huu zikiwa na morali ya juu baada ya kufuzu kutoka hatua ya robo fainali iliyochezwa Aprili 23, 2026:

  • Mlandege iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Singida Black Stars
  • Simba nayo ikafanikiwa kutinga hatua hii kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mafunzo

Mlandege imeendelea kuwa mwakilishi pekee wa Zanzibar katika hatua hii baada ya timu nyingine za visiwani kushindwa kusonga mbele.

Historia Inayoibeba Mchezo Huu

Mchezo huu unaingia na uzito wa kipekee kutokana na rekodi za nyuma:

Mwaka 2023, Simba iliondolewa na Mlandege kwa mikwaju ya penalti katika nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya sare ya 1-1
Mwaka 2024, Mlandege iliibuka tena na ushindi wa 1-0 dhidi ya Simba katika fainali ya mashindano hayo

Matokeo haya yanaifanya Simba kuingia uwanjani ikiwa na shinikizo la kulipa kisasi cha kihistoria, huku Mlandege wakilenga kulinda rekodi yao bora dhidi ya wapinzani hao.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. matokeo ya Azam FC vs Yanga SC Leo 25/04/2026
  2. Ratiba ya Nusu Fainali Kombe la Muungano 2026
  3. Timu Zilizofuzu Nusu Fainali Kombe la Muungano 2026
  4. Vilabu Bora Afrika 2026/2027 (CAF Club Ranking)
  5. CAF Rankings 2026: Simba Yaporomoka, Yanga Yaendelea Kung’ara Afrika
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo